Mohammed Hussein Zimbwe Jr, Tuambie Kituo Kinachofuata

July 16 1986 kule cardif Wales alizaliwa Gareth Bale (mkombozi) akiwa mchanga sana baba yake mzee Debbie Bale alimpeleka katika shuke moja ya kanisa la Whitchurch ili apate elimu ya dini na maarifa ya soka.

Alipopata mafunzo ya kutosha, bale akachagua kucheza nafasi ya beki wa kushoto katika maisha yake. Ikawa hivyo mpaka alipojiunga na Southampton mwaka 2006, na 2007 Bale akajiunga na Tottenham Hotspur kama beki mchanga kabisa EPL na kucheza miaka 6 kama beki.

Bale na Villas Boas

Mwaka 2012 kocha wake Andre Villas Boas akamuita pembeni na kumshawishi ahame namba na kucheza kama winga kutokana na uwezo wake mkubwa. Tangu hapo bale akawa wamoto kweli kweli. Uwezo wa bale umenirudisha mpka Bunju pale Mo simba Arena kuitazama miguu ya Mohammed Hussein.

Mwalimu Amunike alimtumia kama winga pale Taifa stars lakini Sven vanderbroek anamtumia kama beki, Binafsi napenda kumuita GENERATOR, ameutawala upande wa kushoto kwenye ramani ya Tanzania, nanyoosha kidole cha shahada kushuhudia ufalme wa Zimbwe kwenye kiti cha enzi juu ya nyasi za Tanzania. Itoshe kusema inatosha Zimbwe kucheza Tanzania.

Farid Mussa na Zimbwe Jr

🎶Pasi zake temethali, zinatibu na kuenzi, krosi zake manuwari akipiga hakopezi. 🎶.. ooh Zimbwee…Bila shaka huyu ndie mchezaji bora wa raundi ya kwanza kwa Simba msimu huu. Ukiachana na skills zake Zimbwe wa leo sio wa jana. Ameimarika kwenye kukaba na kulinda. Wapo wanaokaribia uwezo wake lakini wanatakiwa kujifunza mengi kupitia yeye.

Yupo Edward Charles Manyama wa Namungo, yupo Yasin Mustafa wa Yanga na Bruce Kangwa wa Azam. Hawa wote ni mafundi wenye haiba ya kufanana na Zimbwe Jr. Wakijinoa zaidi basi Ligi yetu itanawiri sana upande wa kushoto.

Bruce Kangwa

Asante kwa burudani Zimbwe. VPL imekufungulia dunia, sasa ni kazi yako wewe kuwa unachotaka. Sitashangaa kukuona ukicheza Ulaya mahala penye hadhi kwako, ila nitaumia nikikuona unastaafu ukiwa Tanzania, na hiyo ndio itakua tafsiri ya dhambi ya usaliti. Chonde chonde usije kutusaliti. Go Zimbwe go.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

12 Komentara

    Makala nzuri

    Jibu

    Asant kwa taarifa meridian bett

    Jibu

    Bonge la makala hipo vizuri

    Jibu

    Makala iko poa sana

    Jibu

    Goodupdate

    Jibu

    Asante kwa makala nzuli

    Jibu

    Mnatujuza meng kwakwel

    Jibu

    Zimbwe saf sana

    Jibu

    Kijana yupo vizuri sana

    Jibu

    Zibwe yupo vizuri sana

    Jibu

    Hussein yuko poa sana

    Jibu

Acha ujumbe