Nyota wa Aston Villa, Morgan Rogers, hana pingamizi lolote la kurejea Manchester City ikiwa atapewa nafasi hiyo, kwa mujibu wa ripoti ya TEAMtalk.

Rogers alifunga mabao 10 katika Premier League kwa mara ya kwanza msimu huu pamoja na kutoa pasi 7 za mabao, huku Aston Villa wakihakikisha nafasi ya kucheza UEFA Champions League baada ya kumaliza katika nafasi ya nne. Kiungo huyo mshambuliaji pia aliisaidia Villa kutwaa UEFA Europa League, akichangia mabao 3 na pasi 5 za mabao, ikiwemo bao alilofunga kwenye fainali.
Si ajabu kwamba kiwango chake kimevutia baadhi ya vilabu vikubwa duniani. Mabingwa wa Premier League, Arsenal FC, wanaripotiwa kuvutiwa naye, huku ikidaiwa kuwa kocha Mikel Arteta ameiomba bodi ya Arsenal kumsajili.
Hata hivyo, Arsenal wanaweza kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Manchester City, klabu ambayo Rogers alitokea katika akademi yake. Ripoti hiyo inaeleza kuwa Rogers yuko wazi kuhusu mustakabali wake ikiwa ofa itatokea, na kwamba nia ya Manchester City ni ya kweli. Aidha, asingekuwa na tatizo lolote kurejea Etihad ikiwa City wataamua kuendeleza harakati zao za kumsajili.
Baada ya kumuuzia Jack Grealish Manchester City mwaka 2021 kwa pauni milioni 100, Aston Villa wanadaiwa kutaka kiasi kikubwa zaidi kwa Rogers, ambaye anaonekana kuwa na sifa zinazofanana na nyota huyo wa zamani wa Villa.
Bado haijulikani kama Manchester City, Arsenal au vilabu vingine vinavyomfuatilia kama Chelsea, Bayern Munich na Paris Saint-Germain vitaafiki mahitaji ya kifedha ya Aston Villa.



