Moto wa Liverpool Balaa!

Ligi kuu nchini Uingereza iliendelea mwishoni mwa wiki hii ambapo ilishuhudiwa mechi kubwa sana katika ligi hiyo kati ya Liverpool waliokuwa wenyeji wa Arsenal ndani ya mechi hiyo. Mechi kati ya klabu hizo ilitawaliwa na ufundi wa aina yake ambapo kila mmoja alikuwa akitafuta nafasi ya kusonga mbele kukiwa ni ile hatua ya kuwinda alama tatu muhimu ambazo zitasaidia kuibuka washindi wa kombe hilo.

Liverpool walionekana mbogo katika mchezo huo kwa kupeleka mashambulizi yaliyokuwa ya kasi sana upande wa Arsenal jambo lililowapa Arsenal mgandamizo mkubwa sana ndani ya mechi hiyo. Uwepo wa hali hiyo na aina ya mchezo waliokuwa wakicheza walinzi wa Arsenal wakashindwa kabisa kuhimili vishindo vya mashambulizi ndani ya mechi hiyo.

Ushindi huo wa 3-1 ndani ya mechi hiyo unawafanya Liverpool kukaa kileleni mwa ligi hiyo huku wakiwa na safari inayoonekana kuwa nzuri kuelekea ubingwa. Nafasi kubwa kwao ni kwa sababu jirani yao Manchester alishindwa kuwika katika mechi yake iliyopita dhidi ya Tottenham hivyo kuwaruhusu Liverpool kukaa juu wakiwa na alama zote ambazo wamezikusanya ndani ya mechi walizozicheza.

Ndani ya mechi hiyo, Salah alishuhudiwa akiweka magoli mawili ndani ya nyavu za Arsenal akiongezea katika idadi ya magoli hayo kutokana na lile la utangulizi lililofungwa na Matip. Walinzi wa Arsenal walionekana kupotea uwanjani jambo ambalo liliwafanya wapinzani wao kutawala mechi hiyo na kufanikiwa kuondoka na ushindi huo.

Lakini baada ya mabadiliko kadhaa yakiwemo yale ya Torreira na Lacazzette mechi iliweza kubadilika kwa kiasi fulani na kuonekana wote wakiwa wanashambuliana kwa zamu. Huku Arsenal akipata nafasi zaidi kwa kipindi kirefu lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Liverpool uliweza kuhimili mashambulizi hayo japo baadaye waliweza kuwaruhusu Arsenal wapate goli moja ambalo zilikuwa ni jitihada za Torreira.

Klopp alipozungumza baada ya mechi hiyo amewasifu nyota wake wote kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha ndani ya mechi hiyo na kusema hakuna mchezaji aliyecheza chini ya kiwango chake, wote walikuwa katika uwezo anaoufahamu. Akamzungumzia Firmino kwamba ana furaha sana kuwa na nyota wa aina yake kikosini.

2 Komentara

    safi sana liverpool

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe