Mchezaji Mason Mount amedhamiria kushinda taji la ndani ya Uingereza na Chelsea baada ya kujaribu mara tatu na kupoteza katika fainali zote.
Kinda huyo ambaye ni zao la akademi ya Chelsea tayari ameshinda mataji makubwa kama Ligi ya Mabingwa, UEFA Super Cup, na Club World Cup.
Msimu huu tayari Chelsea imepoteza fainali ya Carabao Cup dhidi ya Liverpool lakini tayari wamejihakikishia nafasi ya nusu fainali na wamepangwa kucheza dhidi ya upande mgumu Crystal Palace ambayo inasimamiwa na Patrick Vierra huku Wembely mwezi ujao.
“Sote tuna njaa ya ubingwa wa nyumbani. Haijakuwa mbio nzuri zaidi kwetu Wembley lakini tunataka kurekebisha makosa.
“Tayari tumekuwa na fainali moja huko Wembley msimu huu na tumeipoteza kwa hivyo tuna njaa ya kushinda.”
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.