Jose Mourinho anaamini Harry Kane atashiriki kwenye debi ya kali ya kaskazini mwa jiji la London dhidi ya Arsenal licha ya kuendelea kuuguza jeraha ambalo litamfanya mshambuliaji huyo wa Tottenham asiwe kwenye mechi yao ya Ligi ya Uropa na LASK.

Tottenham wanabaki kileleni mwa Ligi ya Premia kwa tofauti ya mabao tu dhidi ya Liverpool licha ya kulazimisha sare ya 0-0 dhidi Chelsea kwenye mechi yao ya mwisho.

Kane alicheza dakika 90 kamili huko Stamford Bridge lakini kunaonekana kuwa shaka kama atakuwa sawa kuelekea dabi dhidi ya Arsenal ambao wanashikilia nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi.

Mourinho: Arsenal Wajiandae Kukutana na Kane

Wakati akiweka wazi kuwa Erik Lamela, Carlos Vinicius na Sergio Reguilon pia wana majeraha, Mourinho aliuambia mkutano wa waandishi wa habari:

“Lamela ana jeraha kwa takribani wiki tatu au mwezi. Siamini kama anaweza kuwa na nafasi wikendi. Harry, Vinicius na Sergio – wanaweza kuwa na nafasi ya wikendi.”

Kuhusu Kane, “Sitakuambia hali ya jeraha lake [Kane]. Nadhani ana nafasi nzuri – ya kucheza dhidi ya Arsenal.”

“Sitaki kusema uwongo, sitaki kuficha chochote kuhusiana na kwamba atacheza au la? Nadhani atacheza. Hiyo ni hisia yangu kwamba atacheza.”

Kane ana mabao saba katika michezo 10 ya Ligi Kuu msimu huu na asilimia 66.67 ya nafasi zake kubwa, kwa data ya Opta.


 

FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Kane, Mourinho: Arsenal Wajiandae Kukutana na Kane, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

21 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa