Ripoti zinasema kuwa Jose Mourinho anajaribu kumshawishi golikipa Gigio Donnarumma kuungana naye pale Roma.
Meneja huyu mpya wa Roma anafanya jitihada za kuandaa kikosi kuelekea msimu ujao 2021-22 na kwa mujibu wa La Gazzetta delo Sport anajaribu kuwapata mastaa bora kutoka sokoni kutimba Serie A.
Taarifa zaidi zinasema kuwa meneja huyu, Mourinho anashauri uongozi wa Roma kujitoa sadaka kwa kuwekeza wachezaji wakubwa wa kimataifa wa Italia.
Donnarumma ni mmoja ya anaowatazama Mourinho. Nyota huyu atakuwa hana klabu ifikapo Julai 1, na mahitaji ya kifedha ya wakala wake Mino Raiola yanawapa shida klabu zinazofikiria kumnunua staa huyu.
Jose anataka wamiliki wa klabu hiyo kufanya kila wawezalo kusaini majina makubwa kwenye soko la soka Italia, uwekezaji ambao bila shaka unaweza kuwapa mwanga kwenye mapambano ya msimu ujao.
Donnarumma ambaye ana miaka 22 kwa sasa anajiandaa na mapambano ya Euro2020 akiwa na kikosi cha Italia, baada ya kufanikiwa kuwasaidia Milan kupata taji lao la pili, akiwa na hati safi 14 kwenye mechi 37 za msimu uliopita.
MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Ampe kishawishi Cha kueleweka sasa