Muite “The Special One”, mtu na nyota yake kwenye ulimwengu wa makocha wa soka duniani. Sio mwingine, ni Jose Mourinho. Hajawahi kuishiwa maneno, safari hii amzunguzia Romelu Lukaku.

Baada ya kufukuzwa Spurs na kutangaza kuwa atakaa nje ya uwanja kwa muda, mambo yalikuwa tofauti. Wiki chache tu baada ya kuondoka Spurs, Mourinho alitangazwa kama kocha mkuu wa AS Roma akichukua nafasi ya Paulo Fonseca ambaye kwa sasa anahusishwa na Spurs kama mbadala wa Jose.

Kwa siku kadhaa sasa, Mourinho amekua akiwazungumzia baadhi ya wachezaji aliowahi kuwanoa na uwezo wao viwanjani kwa sasa. Kwa sehemu kubwa amekuwa akiwazungumzia wachezaji wa Man United na timu ya Taifa ya Uingereza – Luke Shaw, Marcus Rashford, Kyle Walker na sasa ni Romelu Lukaku.

Lukaku alisajiliwa na United akitokea Everton (2018) kwa dau la pauni milioni 75. Ndani ya miaka 4 aliyokaa United alikuwa na kiwango cha kupanda na kushuka kabla ya kujiunga na Inter Milan ambao ameenda kuwa muhimili mkubwa wa timu hiyo kwa miaka miwili ambayo amekuwepo klabuni hapo.

Mourinho

Kama ilivyo kwa wadau na wapenda soka wengi, uwezo wa Lukaku kuzifumania nyavu msimu uliomalizika ulikuwa ni mkubwa sana. Ameisaidia Inter kutwaa ubingwa wa Serie A na kuwavua ubingwa Juventus ambao walikua watawala kwa miaka 9 mfululizo.

Mourinho anakwambia, “[Lukaku] alipokuwa Chelsea alikua ni mtoto, alipokuwa United alikua bado anajifunza lakini akiwa Inter amekuwa mchezaji kamili. Miaka miwili Inter imepatia uwezo binafsi wa kujiamini, kitu ambacho hakua nacho awali. 

“Anapendwa na mashabiki, wachezaji wenzake, kocha na benchi la ufundi. Ni mchezaji mkubwa lakini ana utoto ndani yake. Anahitaji kupendwa, kusaidiwa na kujisikia ni wa muhimu.”


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa