Mourinho: Sijutii Kukataa Kuifundisha Ureno

Kocha wa zamani wa vilabu vya Real Madrid, Chelsea, Man United, Fc Porto, As Roma na Inter Milan Jose Mourinho amefunguka kua hajutii kukataa ofa ya kuinoa timu ya taifa ya Ureno.

Jose Mourinho akifanya mahojiano leo na mwandisho nguli Fabrizio Romano amsema “Nilipata ofa ya kuifundisha timu ya taifa ya Ureno mara mbili mara ya kwanza nikiwa Real Madrid ambapo Rais Perez alikataa, Lakini wakati nipo Roma na miezi michache baadae nilifukuzwa lakini sijutii uamuzi wangu”mourinhoKocha huyo raia wa kimataifa wa Ureno ameweka wazi hayo leo na kusema alikua na nafasi ya kuifundisha timu hiyo kama angekubali ofa yao, Lakini yeye hakuona kama ni jambo sahihi kwa wakati huo kuifundisha timu hivo hana cha kujutia.

Ndani ya Real Madrid kocha huyo alitanabaisha kua alihitajika awe kocha wa Ureno kwa muda na alimfata rais wa klabu Florentino Perez na rais huyo akamueleza hakuna nafasi ya yeye kufanya jambo hilo hivo ilishindikana kuifundisha Ureno.mourinhoKocha Mourinho aliongeza kwa kusema “Sitafurahi kufundisha timu ya taifa labda kama nitapewa ofa hiyo siku chache kabla ya kombe la dunia, michuano ya Euro, Afcon, au Copa America lakini tofauti na hapo sitafurahia kazi kwakua nitahitajika kusubiri miaka miwili tena ya michuano kwasasa hapana labda siku moja huko mbele”

Acha ujumbe