Kwa mujibu wa Tuttorsport, klabu ya Juventus wanaamini kuwa wanaweza wakamnasa kinda machachari wa PSG Kylian Mbappe kwa kuweka sokoni paundi milioni 380! Dau tajwa linaweza kulipa gharama zote za uhamisho na gharama za kusajili mkataba wa miaka mitano.
Raisi Andrea Agnelli na makamu wake Pavel Nedved waliweka bayana baada ya kikao cha wanahisa kuwa mtaji zaidi wa paundi milioni 300 unatarajiwa kuongeza kasi ya Juventus na kuiweka katika vilabu vikubwa zaidi Ulaya.
Mpango wa Juventus katika kuongeza mtaji ni pamoja na khakikisha wanakuwa na uwezo wa kufanya hamisho kubwa zaidi na mastaa wengi wenye uwezo mkubwa kama ilivyo kwa Ronaldo.
jicho la Juventus kwa sasa, baada ya kumchukua Ronaldo ambaye ana miaka 34 ni kumsajili kijana ambaye atakuwa mtaji mkubwa kwa sasa na baadaye.
Kwa mujibu wa Jarida la Tuttospot, Kylian Mbappe ndiye chaguo linalofaa zaidi kwenye aina ya mchezaji ambaye Juventus wanamtaka na wanafanya mipango kwa ajili ya kumnasa.
Mpaka mwezi Disemba, kinda huyu atakuwa na umri wa miaka 21, lakini uwezo wake dimbani umekuwa mkubwa sana na akiwavutia klabu nyingi zaidi za Ulaya. Mpaka sasa akiwa na PSG amecheza mechi 95, amefunga magoli 66 na kutoa usaidizi wa magoli mara 36.
Povel
Habar njema