Baada ya tetesi ya muda mrefu kuwa Simba ingeachana na washambuliaji wake wawili Medie Kagere na Chris Mugalu nmwisho wa msimu huu ghafla mambo yamebadilika na wachezaji hao wanaweza kuwepo katika msimu ujao ndani ya timu hiyo.

 

Mugalu
Mugalu

Mugalu na Kagere msimu uliopita hawakuwa na msimu mzuri mara baada ya kushindwa kufanya vizuri kama msimu wa mwaka 2020/21 ambao walifanikiwa kufunga mabao zaidi ya 25 kwa pamoja.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmedy Ally alisema kuwa wachezaji wote ambao wamekwenda katika maandalizi ya msimu ujao huko nchini Misri watakuwa katika sehemu ya kikosi cha Simba kwaajili ya msimu ujao akiwemo Kagere na Mugalu.

“Wachezaji wote ambao wamekwenda katika maandalizi kwaajili ya msimu ujao na timu huko kambini nchini Misri watakuwa katika mipango ya mwalimu kwaajili ya msimu ujao na ndio maana wapo katika safari yetu.

 

“Kagere na Mugalu bado ni wachezaji wa Simba na ndio maana wote wapo katika safari ya kwenda nchini Misri kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao,Kagere ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi hivyo bado ni mchezaji halali na atakuwepo,” alisema kiongozi huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa