Muller na Kimmich Wapata COVID-19

Wachezaji wa Bayern Munich Thomas Muller na Joshua Kimmich wamejitenga baada ya kupimwa na kukutwa na virusi vya Corona.

 

Muller na Kimmich Wapata COVID-19

Taarifa hizo zilitoka baada ya ushindi wao walioupata hapo juzi Ijumaa kwenye mchezo wa Bundesliga walipomkaribisha Bayer Leverkusen kwa mabao 4-0, huku Muller na Kimmich wakiwa katika kikosi cha kwanza.

Mabingwa hao wa Ujerumani walisema kuwa wawili hao walipimwa na kukutwa na virusi hivyo Jumamosi lakini hawakuwa na dalili na wanaendelea vizuri na wamejitenga katika nyumba zao.

Muller na Kimmich Wapata COVID-19

Wachezaji hao wa Bundesliga wanatarajiwa kuvaana na klabu ya Czech, Viktoria Plzen katika Ligi ya Mabingwa katika Uwanja wa Allianz Arena siku ya Jumanne.  Kimmich ameanza kila mechi katika michuano yote msimu huu akiwa na Bayern, akifunga mabao mawili na kutoa pasi nne za mabao.

Muller ameanza katika mechi zote za Bayern katika michuano yote, akifunga mara mbili na kutoa asisti nne.

Muller na Kimmich Wapata COVID-19

 

Acha ujumbe