Andy Murray amejiondoa kwenye pambano lake la hatua ya 16 bora dhidi ya Novak Djokovic kwenye michuano ya Madrid Open kutokana na kuugua.

Taarifa kwenye mtandao wa Twitter wa mashindano hayo ilisomeka: “Kwa bahati mbaya, Andy Murray hawezi kwenda kwenye Uwanja wa Manolo Santana kutokana na ugonjwa.”

 

Andy Murray

Murray aliwaondoa Dominic Thiem na Denis Shapovalov na kutinga hatua ya 16 bora, alipangwa kukutana na Djokovic kwa mara ya 37 kwenye ziara hiyo na ya kwanza tangu 2017.

Raia huyo wa Scotland alisema baada ya ushindi wake wa seti tatu dhidi ya Shapovalov haupaswi kuwa na nafasi dhidi ya Djokovic, akidai mchezaji huyo ni namba 1 duniani.

Murray alipokea wildcard kwaajili ya Madrid Open, baada ya awali alipanga kutocheza katika viwanja vya udongo ili kujiandaa kwa kampeni ya viwanja vya nyasi.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa