Bondia wa Masumbwi Nchini, Hasani Mwakinyo amesema hakatai kucheza na mabondia wa ndani kwa kuwa yeye ni bora zaidi ila ni kwasababu anahitaji point zaidi.

 

“Ninachomaanisha mimi ni kwamba, pointi ninazozihitaji ili kunifikisha mahali ninapopataka, kwa Afrika hakuna bondia ambaye anapointi ninazozihitaji. Kama atakuwepo nitapigana.” alianza Mwakinyo.

 

“Sipigani tu ilimradi napigana! Lengo langu sio kupigana tu, napigana lakini nina safari yangu nataka kufika na pointi ndio zitanifanya nifike huko. Ndicho nachomaanisha mimi.

 

“Hofu inakuwa kubwa zaidi nikicheza nyumbani kwa sababu ma-promoter wanaotuandalia mapambano bado hawana hisia ambazo tunazo sisi wachezaji. Ndio maana Ulaya kila bondia ana promoter wake.”  Mwakinyo alisisitiza

 

“Kwa mfano mimi nipo namba 5 kwenye viwango vya mabondia, nataka kufika namba 20 duniani, natakiwa kucheza na bondia mwenye rekodi ambayo itaweza kunifikisha huko juu. Bondia huyo anataka dola 25,000 lakini promoter anayeandaa pambano bajeti yake ni dola 3,000.

 

“Kwa hiyo hata nikifika namba 20 kwenye ubora nitatumia muda mrefu kwa sababu nacheza na watu ambao sio rank yangu hawana pointi za kunipandisha. Kwa hiyo badala ya kupata 10 pointi nisogee juu inabidi nizichange.

 

“Kwa hiyo unacheza lakini unakuwa kwenye hatari, badala ya wewe kupanda unaweza ukapigwa halafu ukashuka zaidi ukampandisha mtu wa chini yako. Unapocheza na mtu kwao unacheza na bingwa, ukipigwa haitashangaza watu na ukishinda upanda kutoka kwa bingwa.

 

“Bondia niliyechezanae juzi ni mzuri lakini alikuja kwa sababu bondia ambaye nilitakiwa kupigananae hakuweza kuja kwa hiyo nisingepigana siku ile ingeonekana watu wamedanganya umma kwamba wametangaza nitacheza halafu sijacheza.

 

“Kiuhalisia hakustahili kucheza na mimi kwa hiyo nikakatwa pointi mbili kwa kukubali kucheza na bondia yuko chini ya rank yangu. Kupigananae haijaniongezea, imenitia hasara. Nashukuru nimechukua mkanda ambao unaweza kunisogeza sehemu nyingine.”aliongeza Mwakinyo

Ni bora promoter sikukipe pesa lakini akakuletea bondia mwenye rank ya juu, kuliko akulipe pesa nyingi halafu akuletee bondia wa rank ya chini.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa