Baada ya kutoka kichwa chini mbele ya Lambalamba Azam FC, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ameanza mikakati mipya na safu yake ushambuliaji kutokana na kukosa umakini wa kutumia nafasi wanazotengeneza.

Kwa mujibu wa kocha wa makipa wa Yanga, Razak Siwa, alisema Nabi amewaambia wachezaji wake anataka soka la kushambulia na washambuliaji kuongeza umakini na utulivu wanapopata nafasi uwanjani.

“Sasa kila mchezaji amepewa majukumu yake ya kuhakikisha tunaenda kufanya vizuri kwenye mechi ijayo ya FA, hasa umakini kwa safu ya ushambuliaji kwa kutumia vema nafasi wanazotengeneza uwanjani,” alisema Siwa.

“Kitendo cha kupoteza mechi yake ya kwanza hakupendezewa nacho, amewaambia hataki soka la kubutua butua na kila mmoja apambane kwa maslahi ya timu ili kufikia malengo yao.”

Yanga kesho Ijumaa itashuka Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa kuvaana na wenyeji, Tanzania Prisons kwenye mechi ya robo fainali Kombe la FA.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

12 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa