Nabi : Hatuzungumzii Matokeo ya Timu Nyingine.

 

Kocha wa Kikosi cha Yanga SC, Mohamed Nabi amesema amewapiga marufuku wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo kuzungumzia matokeo mabovu ya watani wao Simba Sc ambayo wamekuwa wakiyapata katika mechi zao za hivi karibuni na badala yake wajikite katika michezo yao na kuhakikisha wanashinda.

 

“Nimewaambia wachezaji sitaki kusikia hata wanazungumza kuhusu Simba kwani matokeo yao hayatuhusu na nimewataka wazingitie na kufikiria zaidi mechi zetu zinazotukabili.

“Nimewaambia kabisa nikimkuta mchezaji yeyote anafanya hivyo au mtu yeyote katika benchi langu la ufundi akiijadili Simba au timu nyingine juu ya matokeo yao nitawapa adhabu zilizopo kwenye miongozo yao ya kazi.

Yanga tuna mechi zetu ambazo sasa zitazidi kuwa ngumu, nimewaambia kuanzia sasa kila mchezo utakaokuwa mbele yetu utakuwa ni sawa na fainali ngumu ambazo ni lazima tuzishinde,”- aliongeza Nabi.

Simba SC katika michezo mitatu ya mwisho ya Ligi wamecheza dakika 270 bila kufunga bao wala kushinda huku akifungwa mechi mbili, ya Mbeya City na ile ya Kagera na kutoa sare mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe