Kocha wa klabu ya Bayern Munich Julien Nagelsman Amefanikiwa amefurahishwa kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake katika mchezo uliopigwa jana usiku dhidi ya Fc Barcelona katika dimba la Camp Nou.

Klabu ya Fc Bayern jana walifanikiwa kupata ushindi wa magoli matatu kwa bila wakiwa ugenini dhidi ya Barcelona na kuitupa klabu hiyo nje ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa misimu miwili mfululizo.nagelsmanKocha Nagelsman anasema wachezaji wake wakicheza vizuri katika mchezo huo na kusema wanahitajika kucheza vizuri katika maeneo yote huku akionekana kufurahishwa zaidi na kucheza na klabu ya Barcelona kwa dakika 94 na kutokuwaruhusu Barcelona kupiga shuti lililolenga lango.

Fc Bayern wamefanikiwa kufuzu ya 16 bora wkiwa kama kinara wa kundi C wakiwa na alama 15 kwani wameshinda michezo yote mpaka sasa kwenye kundi hilo.nagelsmanKocha Nagelsman anaivusha Bayern kwenye hatua hiyo kw mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivo msimu uliomalizika lakini wakiishia kutolewa katika hatua ya Robo fainali dhidi ya Villarreal.

Barcelina wao wataelekea kwenye michuano ya Uefa Europa league baada ya kupokea kichapo jana usiku ambacho kilihitimisha matumaini yao ya kendelea kusalia katika ligi ya mabingwa barani ulaya.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa