Kocha mkuu wa Bayern Munich Julian Nagelsman amesema kuwa lazima ‘afikirie kila kitu” baada ya kuona timu yake ikipoteza mchezo wa jana ambapo walikuwa ugenini wakikipiga dhidi ya Augsburg ambapo walipoteza kwa bao 1-0.

 

Nagelsman: "Nafikiria Juu ya Hali Yangu"

 

Bao la Mergim Berisha ambalo lilifungwa katika kipindi cha pili ambalo lilifungwa katika uwanja wa Augsburg Arena liliifanya Bayern kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa msimu huu, huku kupoteza mchezo huo kulifanya mabingwa watetezi hao kuwa ni mechi ya nne ambayo hawajapata matokeo baada ya kupata sare tatu mfululizo mechi zilizopita ambapo walifanya hivyo tangu 2001/2002.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na boss wa Augsburg Enrico Maassen baada ya mchezo huo, Nagelsman aliwasifu washindi hao huku akiamini timu yake bado ilipaswa kushinda mchezo huo.

 

Nagelsman: "Nafikiria Juu ya Hali Yangu"

“Hongera Augsburg na Enrico kwa ushindi wao dhidi yetu,” Alisema. Nikiangalia takwimu nadhani tulipaswa kushinda mchezo huo, ikiwa tutalinda vizuri mpira wa adhabu uliosababisha bao.”Ilikuwa ngumu kuwavunja baada ya kwenda 1-0″

Nagelsman aliendelea  kuongea huku akisema kuwa hatamzungumzia mchezaji mmoja mmoja bali ataongea na wachezaji wote  moja kwa moja ambapo aliongelea pia suala la kukosa namba 9 na kusema kuwa hata akisema mtafanya nini. Na mwisho akasema anafikiria kuhusu hali waliyonayo na anajifikiria yeye pia ambapo walijaribu kupiga mashuti mengi lakini golikipa wa Augsburg aliyacheza vizuri.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa