Nagelsmann Anasikilizia Dili Jipya Ujerumani

Kocha wa zamani wa vilabu vya Rb Leipzig na Bayern Munich ambaye kwasasa anafundisha timu ya taifa ya Ujerumani Julian Nagelsmann amesema anasikilizia dili jipya ndani ya timu hiyo.

Nagelsmann ambapo alipewa mkataba wa kuiongoza timu ya taifa ya Ujerumani mpaka kumalizika kwa michuano ya Euro mwaka huu yatakayopigwa nchini humohumo, Kocha huyo ameeleza uongozi ndio una kazi ya kufanya juu ya suala la yeye kuendelea kuifundisha timu hiyo.nagelsmannKocha huyo amesema kuna mambo yanayofuatiliwa kwa karibu na uongozi ambao ndio waliompa kazi kocha yeye, Hivo mwisho wa siku wao ndio wataamua yeye kama anafaa kuendelea kua kocha wa timu hiyo lakini haitahusiana na suala fedha kabisa.

Kocha Nagelsmann amekua na mwendelezo mzuri mpaka sana tangu achukue kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani, Jambo ambalo limewavutia shirikisho la soka la Ujerumani kutaka kumpa mkataba mpya kocha huyo.nagelsmannKocha huyo wa zamani wa Bayern Munich licha ya kua kwenye mipango ya shirikisho la soka Ujerumani na kutaka aendelee kuinoa timu hiyo, Lakini wakati huohuo vilabu mbalimbali vinaelezwa kuvizia saini ya kocha huyo wa kimataifa wa Ujerumani

Acha ujumbe