Nagelsmann: Bayern Walipaswa Kufunga Zaidi.

Kocha mkuu wa Bayern Munich Julian Nagelsmann amesema kuwa timu yake ilipaswa kufunga zaidi hapo jana kwenye ushindi wao wa 5-2 ugenini dhidi ya Augsburg katika raundi ya pili ya DFB-Pokal.

 

Nagelsmann: Bayern Walipaswa Kufunga Zaidi.

Klabu ya Bayern ilitanguliwa kufungwa bao ndani ya dakika 9 za mchezo na baadaye Choupo Moting akasawazisha bao hilo dakika ya 27, akiongeza lingine, mabao mengine yalifungwa na Joshua Kimmich, Jamal Musiala pamoja na Alphonso Davies.

Licha ya kufunga mabao matano dhidi ya Augsburg, Nagelsmann alitaka timu yake isiwe na huruma zaidi, akiiambia ZDF: “Ni mchezo wa kombe la kawaida timu ilitengeneza nafasi za kutosha ili kufanya mchezo uwe wazi mapema, lakini kwa bahati mbaya tulikosa.

Nagelsmann alisema kuwa kulikuwa na hali nyingi ambazo walipaswa kufunga mabao zaidi na pia alishukuru kwa kuimarika kwa kikosi chake baada ya kujipatia bao la kwanza mapema hasa baada ya kurudi mapumziko.

Nagelsmann: Bayern Walipaswa Kufunga Zaidi.

Kocha huyo aliendelea kwa kusema kuwa hawakuwa na mwanzo mzuri, walikuwa wavivu sana dakika 20 baada ya kipindi cha mapumziko zilikuwa nzuri sana huku akisema kuwa kimwili walikuwa kwenye kiwango sawa.

Nagelsmann alipoulizwa kwanini timu yake ilianza vibaya alijibu kuwa sio rahisi sana kucheza dhidi ya timu ambayo inacheza kila mpira mbele moja kwa moja.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.