Zidane hajaanza kwa kufanya vyema sana kama matarajio ya wengi toka aliporejea kikosini hapo. Mashabiki wamepoteza imani na baadhi wakishinikiza meneja huyu atimuliwe klabuni hapo. Tetesi zimewataja wataalamu ambao wanaweza kuichukua nafasi ya meneja huyo, hapa kuna orodha ya wanaotarajiwa ikiwa Zidane atatimuliwa;
Jose Mourinho: Aliyekuwa meneja wa Manchester United ambaye bado hajapata kibarua toka alipotimuliwa klabu ya Manchester United, anatajwa kuwepo kwenye orodha ya wanaotarajiwa kuichukua nafasi hiyo. Anatarajiwa akirejea klabuni hapo huenda akafanya makubwa kubadilisha hali na ugumu wanaopitia klabu hiyo.
Massimiliano Allegri: huyu alishawahi kutajwa kwenye orodha ya waliokuwa na nafasi ya kuchukua kinbarua hicho mwaka 2018 baada ya Zidane kuondoka. Allegri, Antonio Conte and Mauricio Pochettino wote walitajwa kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuchukua kibarua hiki kabla hawajapigwa gepu na Julen Lopetegui. Kwa sababu sasa hana mkataba na Juventus, huenda nafasi yake ikawa ni baada ya Zidane kuvurunda.
Raul Gonzales: Huyu ni kepteni wa zamani wa Real Madrid ambaye alifanikiwa kuingia kikosi cha kwanza baada ya Rafael Benitez kufukuzwa. Anatarajiwa anaweza kuwa na nafasi kama ilivyokuwa kwa Santiago Solari ambaye aliitwa kumbaadili Lopetegui msimu uliopita.
Edgar
yani hapo wakitaka afanye vzr kwanza angerudi ronald