Safari ya Maurizio Sarri akiwa na Chelsea huenda akawa imefika mwisho kama meneja huyu kweli ataamua kusepa klabuni hapo. Henda kwa mara nyingine angeweza kuwarejesha Chelsea kwenye Ubingwa wa Ulaya na kushinda Ligi ya Europa lakini dondoo zinaonesha uwezekano mdogo mnno wa meneja huyu kusalia klabuni hapo.
Meneja huyu ambaye ni raia wa Italia, hajaweza kufanikiwa kuteka hisia za mashabiki wote wa Chelsea, baadhi yao wanataka meneja huyu aondoke klabuni hapo wakimlaumu kwa Chelsea kutofanya kama walivyokuwa wakitarajia. Jitihada za Chelsea msimu uliokwisha zimeishia kuwaweka kwenye nafasi ya tatu, nyuma ya Manchester City na Liverpool.
Wanachelsea walikuwa na matarajio na staili ya soka ya Sarri, ambayo ni maarufu kama “Sarri Ball” na matarajio yao yalitoweka ghafla baadaya kichapo kikubwa kutoka wa Manchester City na Bournemouth.
Dondoo hasa kutoka katika vyanzo vya habari za michezo Italia, zinamtaja meneja huyu yuko mbioni kuelekea Italia kama meneja ajaye wa Juventus ndani ya Serie A.
Nani mwenye nafasi kubwa kuuvaa umeneja Chelsea?
Swali ni je Chelsea wanamtarajia nani kama meneja? Fununu zina wazungumzia hawa;
Frank Lampard: Lampard anaweza kupata sapoti kuto kakwa klabu, wachezaji na mashabiki kutokana na Historia yake dhidi ya klabu hii, lakini kuna shida katika suala la uzoefu wake kama meneja akiwa na mwaka mmoja tu kama meneja Derby County.
Massimiliano Allegri: Ameweza kutawala Serie A akiwa kama meneja wa Juventus na kushinda Serie A mara 5. Pia ameshinda mataji 4 ya Coppa Italia na kuwafikisha mabingwa wa Serie A Juventus kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa mara 2.
Mameneja wengine wanaotajwa kwenye orodha hii, ambao mmoja wao anaweza akavivaa viatu vitakavyovuliwa na Maurizio Sarri ni; Patric Vieira, Jose Mourinho, Nuno Espirito Santo, Steve Holland, Erik Ten Hag, Laurent Blanc, Julen Lopetegui, Ernesto Valverde.
Povel
Gud news