Nani Zaidi? Drogba Ama Eto’o?

Jiji la London ni miongoni mwa majiji mashuhuri duniani. Linapatikana katika nchi ya Uingereza. Ukipata fursa ya kutembelea jiji hilo hasa maeneo ya Fulham basi hakikisha unapita sehemu hizi: kama wewe ni mpenzi wa maakuli usiache kupita Ice and Slice Restaurant, hapa utapata vyakula vya asili vya Uingereza. Hautojutia muda wako. Kama wewe ni mpenzi wa vito vya thamani kama pete za dhahabu, hereni au bangili basi Circa Vintage ndo’ chaguo lako sahihi. Na kama wewe ni mpenzi wa soka, bado hujazuru Fulham London vya kutosha kama utaondoka hapo bila kutembelea makao makuu ya timu kubwa Uingereza na duniani kwa ujumla, Chelsea FC.

Chelsea ni timu yenye historia kubwa tangu kuundwa kwake mwaka 1905. Ukongwe wa timu hiyo unafanya kuweko historia kadhaa ambazo zinawekwa na kusahaulika klabuni hapo, lakini kamwe hapatotokea kusahaulika miaka ya dhahabu ya mshambuliaji wao hatari Didier Drogba.

Nyota huyo mwenye asili ya Afrika amejijengea heshima yake ndani ya klabu ya Chelsea na anaendelea kuheshimika na mashabiki hata viongozi mpaka leo. Mashabiki hao hawatomsahau John Terry, hawatomsahau Frank Lampard. Lakini kwa gharama yoyote watazidi kumkumbuka Didier Drogba. Jamaa alikua anajua wajibu wake wa kufunga magoli, yeye akaifanya hiyo kuwa ni sehemu yake ya maisha. Kufunga!

Ukitaka kuona ukomo wa hasira za mashabiki wa Chelsea waambie Drogba hakuwa bora, lakini ukitaka kuona hasira zao zikivuka mipaka we’ jaribu kushindanisha Grogba na mchezaji mwingine wa zama zake. Tena ukitaka uwakere zaidi mpe ushindi huyo mchezaji wako mwingine, hawatokuelewa!

Nyota mwingine wa zamani wa Barcelona Samuele Eto’o ametaka kuziona hasira hizo, Eto’o amenukuliwa na mtandao wa Goal akisema yeye alikua bora kuliko El Hadji Diouf na Didie Drogba. Mashabiki wa Chelsea mnasemaje hapo?

Eto’o alisema hayo akimjibu Diouf ambaye siku kadhaa zilizopita alichapisha video  katika mitandao ya kijamii akijigamba kiwa yeye ndio mchezaji bora wa muda wote Afrika. Drogba na wachezaji wengine wakubwa Afrika bado hawajajibu hili lakini Eto’o hajataka kuliacha lipite.

“Hakuna hata mmoja kati yao (Drogba na Diouf) aliyekuwa anafikia uwezo wangu au kunizidi, katika maisha yangu yote ya soka nilitaka kuwa namba moja na kwa hakika ilikuwa hivyo” Eto’o.

Ni kweli kuwa Eto’o alikua namba moja katika maisha yake yote ya soka? Mimi nakupa takwimu jibu utatafuta mwenyewe. Tena kaa nalo usimwambie mtu.

Etoo alichezea vilabu vikubwa Ulaya kama vile Inter Milan, Barcelona na Chelsea. Elishabeba tuzo ya mchezaji bora Afrika mara nne, na akawa mshindi namba tatu katika tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa dunia mwaka 2005 nyuma ya Ronaldinho na Lampard.

Akiwa Barcelona alibeba La Liga mara tatu, Copa Del Rey mara moja, na kombe la ligi ya mabingwa Ulaya mara mbili.

Akiwa na Inter Milan alifanikiwa kuchukua taji la Seria A mara moja, Coppa Italia mara mbili mfululizo, ligi ya mabingwa Ulaya ‘UCL’ mara moja, na taji la FIFA la klabu bingwa ya dunia mara moja.

Mafanikio ya Eto’o hayaishii katika ngazi ya vilabu. Hata ndani ya timu yake ya taifa alishafanikiwa kubeba medali ya dhahabu katika mashindano Ya Olympics yaliyofanyika mwaka 2000, kisha mwaka huo huo akashinda kombe la afcon kabla hajafanya hivyo tena mwaka 2002.

Swali kwa mashabiki wa Chelsea, kwa hizo rekodi za Drogba unazozifahamu je, zinamfanya Drogba kuwa chini au zaidi ya Eto’o? Jiulize kisha majibu kaa nayo.

51 Komentara

    Etoo..!hanajua sana

    Jibu

    Sio mkal tu jamaa anajua tena n mchezaji ambaye aliyelipwa hela nying kwa bara la Africa aliyechezea ulaya

    Jibu

    Etoo ni noma sana

    Jibu

    Etoo yupo vizur “meridianbettz

    Jibu

    drogba juuuuuu

    Jibu

    Etoo anajua

    Jibu

    Didier goal drogba tembo wa ivory coast. Mfalme darajan London yupo juu thanks meridian kwa update

    Jibu

    Eto’o baba lao

    Jibu

    Drogba Yuko juu

    Jibu

    Mnyama Drogba ni balaaa maana aliyoyafanya sote tumeona paleee darajani

    Jibu

    Wote Kama wanalingana Ila eto’o kamzidi kidogo

    Jibu

    Eto’o

    Jibu

    Namkubali Sana Eto

    Jibu

    Eto bonge la kiungo

    Jibu

    Nimchezaj mwenye viwango vyake africa

    Jibu

    Wote Kama wanalingana Ila eto’o kamzidi kidogo drogba kwa sababu eto,o amecheza timu nyinginyingi

    Jibu

    Drogba anatisha

    Jibu

    Drogba ndio zaidi

    Jibu

    Drogoba ni hatari

    Jibu

    Eto yupo vizuri

    Jibu

    Etoo nomaa

    Jibu

    Wachezaji hote niwazuri nahote kila mtu hana upiga mpira nakilamtu akikasehemu yake halio pangwa lazima hai tende kaz

    Jibu

    Eto’o fundiii

    Jibu

    Drogba mkali

    Jibu

    Eto’o baba lao

    Jibu

    Wote wanafanya vizuri sana kwenye soka

    Jibu

    Drogpa ni habari nyingine

    Jibu

    Eto’o hana mpinzani

    Jibu

    Mote wakali

    Jibu

    Hii nimeipenda

    Jibu

    Etoo mkali

    Jibu

    Anajijua na anauwezo mzuri Eto’o wewe ni hatariii

    Jibu

    Wote mafundi

    Jibu

    Mmmmh! ila Eto’o mkali aise

    Jibu

    Mmh kwan huyo Drogba alikuwa anamiguu minne?

    Jibu

    drogba namkubali yuko vzr

    Jibu

    Eto’o Mkali hapa hana mpinzani na ukweli ni kama antena juu wa bati ipo wazii tuu.

    Jibu

    Drogba noma sana

    Jibu

    Eto’o yuko vizuri sana ni 🔥🔥🔥

    Jibu

    Etoo #meridianbet

    Jibu

    Aisee mmenitajia mgahawa wangu Ice and slice Restaurant daa nishakula na drogba hapa #Meridianbettz

    Jibu

    Etoo ni mkali kuliko na anakiwango cha juu

    Jibu

    Kimafanikio etoo hana mpinzani katika Africa

    Jibu

    Etoo yuko vizuri kuliko

    Jibu

    Samwel etoo # meridianbettz

    Jibu

    etoo tupo vzr

    Jibu

    Etoo alikuwa zaidi ila majibu yangu ndugu mwandishi umenambia nikae nayo

    Jibu

    Wote nawakubali ila etoo jembee sanaaa

    Jibu

    Etoo ni alikua zaidi ya wote hao..

    Jibu

    Etoo ni alikua zaidi ya wote hao..

    Jibu

    Wote wakali Sana etoo mkali pia ht drogba mkali kiukweli wamesaidia San timu zao

    Jibu

Acha ujumbe