Klabu ya Napoli imefanya kile kilichotarajiwa na wengi baada ya kubadilisha jina la uwanja wao na kuupa jina la Diego Maradona ambaye alikuwa mchezaji wa timu hiyo.

Mchezaji wa zamani wa Napoli ambaye pia aliitumikia timu ya Taifa ya Argentina kama mchezaji na baadaye kuwa kocha – Diego Maradona, alifariki dunia mwezi Novemba, 2020 akiwa na umri wa miaka 60.

Maradona ni mchezaji aliyeipatia umaarufu na mafanikio makubwa klabu ya Napoli ambayo aliitumikia kwa muda mrefu na kuipatia mataji mawili ya Serie A mwaka 1987 na 1990.

Napoli, Napoli Wampatia Heshima Diego Maradona., Meridianbet
Diego Maradona Alipokuwa mchezaji wa Napoli.

Jina la zamani la Stadio San Paolo sasa litabadilika na kuitwa Stadio Diego Armando Maradona hii ni baada ya taratibu zote za kubadilisha jina kukamilika na kuidhinishwa na mamlaka za mji huo.

Taarifa rasmi kutoka kwenye halmashauri ya mji wa Naples imeripoti “Mabadiliko yalisainiwa na halmashauri yote ya jiji. Maradona ni mchezaji bora wa muda wote ambaye kwa kipaji chake, aliitumikia timu ya Napoli kwa ari kubwa ndani ya miaka 7 na ataendelea kupendwa daima.”

Napoli, Napoli Wampatia Heshima Diego Maradona., Meridianbet
Stadio San Paolo sasa kuitwa Stadio Diego Armando Maradona

Maradona aliitumikia klabu hiyo katika michezo 188 hii ikiwa ni idadi kubwa ya michezo aliyoitumikia klabu hii ikilinganishwa na vilabu vingine alivyopitia katika maisha yake ya soka.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Napoli, Napoli Wampatia Heshima Diego Maradona., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

21 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa