Michezo iliyobakia ya kukamilisha msimu wa kikapu huko Marekani #NBA inawezwa kuchezwa kwenye eneo la mapumziko la Disney Frolida kuanzia tarehe 31 Julai.
Msimu wa NBA ulisimamishwa hapo Machi 11 kutokana na janga la Corona. Timu 13 kutoka ukanda wa Magharibi na timu 9 kutoka ukanda wa Mashariki zitachuana katika michezo nane kwa kila timu na kisha kucheza Play-Off.
Mapendekezo ya timu zote 22 za NBA ni kwamba zitacheza katika eneo moja na kuchezwa bila mashabiki ili kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona. LA Lakers, LA Clippers, Denver Nuggets, Utah Jazz, Oklahoma City Thunder, Houston Rockets, Dallas Maverick na Memphis Grizzlies zishafuzu kucheza kwenye Play off kutoka ukanda wa Magharibi.
Milwaukee Bucks, Toronto Raptors, Boston Celtics, Miami Heat, Indiana Pacers, Philadelphia 76ers, Brooklyn Nets na Orlando Magic zimechukua nafasi ya play off kwenye ukanda wa Mashariki.
Timu hizo 16 zitaungana na New Orleans Pelicans, Portland Trail Blazers, Phoenix Suns, Sacramento Kings na San Antonio Spurs kutoka ukanda wa Magharibi na Washighton Wizard kutoka ukanda wa Mashariki.
Tarehe ya hivi karibuni inayotajwa ya kukamilisha msimu huu, ambao ni mchezo wa fainali ya NBA inatajwa kuwa Oktoba 12.
Ester mmakasa
Ni sawa NBA kwa uwamuzi wenu kwasababu ugonjwa bado haujaisha .
Furahav
Hii habari iko poa sana.
Sadick
Nasubiri kuona Kelvin Durant akifanya vitu vyake#meridianbettz
Rehema
Safi sana kwa uwamuzi wenu ugonjwa haujaisha.
mwakalosi
dah lakini sio mbaya,nitasubili ili nione chama from city by the bay golden state warriors
Salma
Safi uwamuzi nzuri
David Pere
Duh! Bila mashabiki Ndio kilichobaki michezo yote Sasa hivi
Samiah
Uwamuzi mzuri sanaaa
Tahiya
Habari njema hii japo bila ya mashabik
Theckla
Tumemisi kikapu
Evaluziga
Safi sana kwa uamuzi wenu ugonjwa bado haujaisha
Adelta
Ni vizuri kwa uamuzi waliofanya
Kwa sababu ugonjwa haujaisha
Hope mwaikuka
Finale mchezo pendwa warud
Neema hassan
Tunasubiri kwa hamu..
Gabriel
Bora maana nilimic sana basketball
Shafii
Kwa mashabiki wa kikapu kazi kwetu Sasa
felister
safi lakini haitonoga bila mashabiki
Asha mvugalo
Asanteni kwa kunijuza
Elika
Itafika mwisho tuu.Nba nawo watakuwa na mashabiki
Ester jackson
Iko powa tutaangalia tu kwa luninga
Antony Luseno
Muda wa kuwaona watu kama lebrone wakifanya mambo yao uwanjani
Rehema Dickson
Ni muda mzuri kwa sisi wapenzi wa nba bado atujachelewa sana tunasubir kuona makal ya wachezaji wetu baada ya kua nje kwa kipindi hicho chote kutokana na janga la corona
Frank Patrick
Always king James Fan …
Mwanaidi
itakuwa poa sana aisee
JULIANA
Wasiwasi ndio akili, NBA wako sahihi gonjwa la corona alijaisha bado tunaishi nalo.
Ernest
Itakuwa pouwa sana
Amani
Toronto Raptors nilimiss Sana hii timu inawachezaji wanao jituma
Zeiyana
Kilichobaki kukubaliana na ali iliyokuwepo mambo yaendelee tu..!tulimic sana NBA
Lydia Emmanuel Magoti
Itakuwa poa sana
Genia Sikaluzwe
Habari njema sana
Theonestina
Wavimilie tu kucheza bila mashabiki.maana hili janga Sio poa
Caroline
Mpira bila mashabiki ata hainogi.lakini hawana jinsi
mathayo sonje
ama kwa hakika dunia inafunguka sasa, maana michezo mingi ilikua imesimamishwa sasa inarejea kumalizia misimu yao ambayo ilikua imebakia. #meridianbet
Kenani
Itanoga kwel bila mashabiki
Neema juma
Kwa ajili ya hili gonjwa sio mbaya kwa maamuzi yao
Mwajuma
Wenye moira wao wa kikapo wanarudi uwanjani sasa
Isaya massawe
Inapendeza kuona michezo mbali mbali ikirudi
Aziza mushi
Safi Sanaa kwa maamuzi.
Povel
Gud news
Mwanahamisi
Asante kwa kunijuza
Mariam mtandama
Safi
Emmy cleopa
Itakuwa vizur sana
Sabrina
Maoni:iko poa hii fresh tu
Blooklyn Nets Yamsajili Mkongwe Beasley.
[…] ya mpira wa kikapu nchini marekani Blooklyn Nets imefanya usajili wa mchezaji wa zamani wa timu hiyo Michaell Beasley ili kuisaidia timu hiyo kunako ligi ya […]