Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije, amekula shavu katika kikosi cha Kiyovu Sports cha Rwanda kutangazwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Ndayiragije amekula shavu hilo kwa kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuinoa timu hiyo ikiwa ni miezi michache baada ya kuvunjiwa mkataba wake ndani ya Stars.

 

ndayiragije, Ndayiragije Atua Kiyovu Sports Rwanda., Meridianbet

Taarifa ambayo ilitolewa na klabu hiyo ilisema kuwa Ndayiragije amepewa mikoba ya kuinoa timu hiyo akichukua nafasi ya Olivier Karekezi ambaye alitimuliwa.

Kocha huyo atakuwepo kwenye kikosi hicho hadi Juni 2023, ambapo moja ya masharti ambayo amepewa ni kushinda ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu huu.

Rais wa Kiyovu, Juvenal Mvukiyehe, alithibitisha kusainiwa kwa Ndayiragije, kwa kupitia tovuti ya Times Sport na alithibitisha kuwa kocha huyo mpya amepewa jukumu la kushinda taji la ligi msimu huu.

“Ana uzoefu mzuri wa ukocha, atasaidia klabu kufikia mengi. Ataendelea kufanya kazi na benchi la ufundi na makocha waliopo hadi mwisho ya msimu,” alisema Mvukiyehe.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

ndayiragije, Ndayiragije Atua Kiyovu Sports Rwanda., Meridianbet

SOMA ZAIDI

9 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa