Baada ya kuandamwa na mashabiki pamoja na wadau mbalimbali wa soka nchini Scotland, kocha – Neil Lenon ameamua kujiuzulu katika nafasi yake ndani ya klabu ya Celtic.
Lenon anaachana na Celtic timu hiyo ikiwa imezidiwa pointi 18 na vinara wa ligi soka nchini humo – Rangers.
Huu ni msimu ambao Celtic wapo hatarini kuvunjiwa historia yao ya kubeba kombe la 10 mfululizo baada ya kubeba kombe hilo kwa misimu 9 mfululizo. Neil Lenon alirejea Celtic Februari 2019 baada ya kocha wa wakati ule – Brendan Rodgers alipoachana na timu hiyo.
Lenon aliiongoza Celtic katika ubingwa kwa misimu miwili mfululizo na sasa nafasi yake itachukuliwa na kocha msaidizi wa timu hiyo – John Kennedy mpaka mwisho wa msimu huu.

“Tumekuwa na msimu mgumu kutokana na sababu mbalimbali, kimsingi inaumiza kuona tumeshindwa kufikia viwango tulivyokuwa navyo kipindi cha nyuma.
“Nilijitahidi kwa uwezo wangu kubadilisha vitu lakini kwa bahati mbaya hatujaweza kufanikiwa kama tulivyotegemea. Ninajisikia fahari kuweza kuwapatia mashabiki wa Celtic mataji. Hii klabu itaendelea kuwa sehemu ya maisha yangu, nitaendelea kuwa shabiki wa Celtic na ninaitakia Celtic kila la kheri.” alisema Lenon.
TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET
BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.
Jambo zuri
Amependa yeye kujiuzuru ni fresh tu
Inapendeza Sana
Safi
Jambo zuri
Eh heri nusu shar kulko shar kamil
Bora alivyojiondoa mapema
Vizuri kwauwamuz aliyo ufanya
Kesha pata ugali kwingine