Beki wa zamani wa Manchester United Gary Neville ameibuka na kudai kuwa kitendo cha Manchester United kumuongeza mkataba straika wao, Edinson Cavani kuwa ni cha malengo ya muda mrefu na kitawasaidia sana.

Mchezaji huyo wa Uruguay ataendelea kusalia OT kwa msimu mmoja zaidi baada ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kusalia United. Cavani amekuwa kwenye kipindi kizuri sana kwenye kuitumikia klabu yake ya Man United katika mashindano yote msimu huu.

Neville

Nahisi ni habari kubwa sana. Nafikiri Cavani amekuwa na kipindi kizuri katika kila mechi aliyopata. Ameonesha ubora wake, uzoefu wake na ana matokeo chanya sana kwa wachezaji wenzake“. Alisema Neville.

Manchester United wanaonekana kushambulia vizuri sana anapokuwa uwanjani, na kitu kizuri sana. Wana mtu mmoja mbele ambaye hawezi kuwaangusha. Amekuwa akiwafurahisha mashabiki na kila mdau wa Manchester United, nafurahi kumuona anaendelea kusalia United kwa ajili ya msimu ujao“, alimalizia Neville.

Cavani ataendelea kusalia United kwa msimu mmoja zaidi na uhakika kuwa atafanya vyema sana. Alipowasili United msimu uliopita, hakuwa na wakati mzuri sana lakini hivi sasa kila mdau anaamini kuwa Cavani yupo kwenye ubora wa hali ya juu.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Neville, Neville Apongeza United Kwa Mkataba Wa Cavani, Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa