Gary Neville na Pier Morgan wamepingana na maamuzi ya Premier League ya kuahirisha michezo yote ya soka nchini Uingereza kwa sababu ya kifo cha Malkia Elizabeth II, saa 24 kabla ya mchezo kati ya Chelsea dhidi Fulhan kwenye mchezo wa wiki ya saba.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United Neville, anaamini michezo yote ya Premier League na michezo ya ligi zingine za Uingereza kuendelea kuchezwa kwa sababu ya ugumu wa ratiba na muingiliano wa mashindano ya kimataifa katika ya ligi kama kombe la dunia.

Neville

Neville alisema maoni yake hayo kwenye mtandao wa twitter wakati akijibu twitter ya Pier Morgan. Morgan aliandika: “Matukio ya michezo yanapaswa kuendelea. A) Malkia alipenda michezo na B) ingekuwa bora kuona au kusikia umati wa watu wakiimba nyimbo ya taifa kutoa heshima zao kwa mtukufu Malkia kama walivyofanya West Ham usiku ubora uliyopita.”

Huku Nevville akiretweet chapisho la Morgan na kukubali. “Nakubaliana na Piers. Michezo inaweza kuonesha vyema kuliko heshima ambayo malkia anastahili”

Michezo yote ya soka nchini Uingereza imeahirishwa na itapingiwa tarehe zingine, wikiendi hii hakuna mchezo wa soka kwe wowote utakaochezwa kwenye ardhi ya Uingereza kwa siku tatu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa