Gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United Gary Neville ambaye kwa sasa ni mchambuzi amesema kua klabu yake hiyo ya zamani haitaweza kumaliza kwenye nafasi tano za juu msimu huu.
Neville ameweka wazi haioni klabu yake hiyo zamani ikimaliza ndani ya nafasi tano za juu msimu huu, Hii ikitokana na mwenendo ambao klabu hiyo imeuonesha mpaka sasa kwenye ligi kuu ya Uingereza.Manchester United wamekua kwenye kiwango kibovu kuanzia msimu huu uanze, Ambapo mpaka sasa wameshapoteza michezo minne ya ligi kuu ya Uingereza ambayo wamecheza huku wakishinda minne kati ya michezo nane.
Beki huyo wa zamani wa klabu hiyo anasema timu hiyo ipo kwenye wakati mgumu sana kwasasa, Lakini akisema mwaka jana Man United walimuumbua baada ya kuwatabiria kua na msimu mbaya baada ya kuanza vibaya na wakamaliza vizuri.Aidha Beki Gary Neville amepigilia msumari kiwango cha golikipa mpya wa klabu hiyo Andre Onana ambaye amekua kwenye kiwango cha chini tangu ajiunge klabuni hapo, Beki huyo anasema ni tatizo kubwa kama golikipa wako namba moja anashindwa kuonesha ubora.