Klabu ya Newcastle United baada ya kutoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa muda mrefu wamerejea kwenye michuano hiyo na kupangwa kwenye kundi la kifo ambalo ni kundi F.
Kundi ambalo klabu ya Newcastle ipo ndio imetafsiriwa na wengi kama kundi la kifo yaani kundi gumu zaidi kwani kwenye kundi hilo kuna vilavu kama PSG, AC Milan na Borussia Dortmund.Kundi hilo linatarajiwa kutokua na mchezo mwepesi wowote kwakua vilabu vyote vilivyopo kwenye kundi F vina uwezo na kuweza kuleta ushindani katika michezo ambayo watakua wanakutana.
Klabu ya Newcastle wamefanikiwa kufanya usajili mzuri kwenye dirisha hili la kiangazi kwajili ya kuboresha timu yao msimu huu na kujitahidi kuendelea walipoishia na kufanya vizuri zaidi msimu huu.Kundi lingine ambalo limeonekana kuvutia watu ni kundi A ambalo lina vilabu vya Manchester United, Bayern Munich, Fc Copenhagen na Galatasaray huku wengi wakisubiri mchezo kati ya Bayern Munich dhidi ya Manchester United.