Imeripotiwa kuwa klabu ya soka ya Newcastle United imeingia katika makubaliano na klabu ya Barcelona kuhusiana na dili lao la winga Philippe Coutinho.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo katika moja ya klabu za ligi kuu ya Ujerumani, Bundesliga, Bayern Munich, anaonekana hatoendelea kukaa kwa Barca wakati ambapo jamaa hao wa Premier League wakiwa wanamvizia ili wamsajili kwao.

Ripoti za hivi karibuni zinasema kuwa nao Arsenal walikuwa wakimuwinda kwa udi na uvumba na huenda wanamsaka mpaka sasa hivi, ila pesa ya kumchukua ambayo ni £300m kutoka kwa Newcastle inaweza kuwafanya The Magpies kuvunja vibubu vyao ingawa kuna shida za kiuchumi kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Coronavirus.

Kwa sasa, Mundo Deportivo wanadai kuwa klabu hiyo ya Steve Bruce imewasiliana na klabu ya soka ya La Liga, Barcelona juu ya uwezekano wa kukamilika kwa dili la Coutinho, ambaye atakuwa naye akihusika katika makato ya mishahara yaliyotokana na matatizo ya kiuchumi katika vilabu vingi duniani.

Mchezaji Coutinho amefunga jumla ya mabao nane na kutoa assists sita kwenye Bundesliga msimu huu lakini mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool anaonekana wazi kuwa hatoichezea klabu ya Bayern kwa mara nyingine kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu.

Klabu hiyo inayoongoza katika msimamo wa Bundesliga walikuwa na chaguo la kumsajili mwanasoka huyo wa kimataifa kutoka taifa la Brazil kwa mkataba wa kudumu lakini waliamua kuachana na dili hilo.

41 MAONI

  1. chaguo la kumsajili mwanasoka huyo wa kimataifa kutoka taifa la Brazil kwa mkataba wa kudumu lakini waliamua kuachana na dili hilo#meridianbettz

  2. Kama Newcastle itahitaji kurudisha heshima yake kwenye ulimwengu wa soka basi Coutinho sio mchezaji wa kumuacha wakati huu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa