Newcastle Yapata Mrithi wa Dan Ashworth

Klabu ya Newcastle United imefanikiwa kupata mrithi wa aliyekua mkurugenzi wake wa michezo Dan Ashworth ambaye amejiunga na klabu ya Manchester United hivi karibuni.

Newcastle United leo imefanikiwa kukamilisha usajili wa mkurugenzi wa zamani wa klabu ya Monaco Paul Mitchell ambaye anakuja kuchukua nafasi ya bwana Ashworth, Mkurugenzi huyo anatarajiwa kuanza kufanya kazi ndani ya klabu hiyo haraka iwezekanavyo.newcastleMkurugenzi Paul Mitchell ambaye amewahi kutumikia klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa kwa mafanikio makubwa, Hivo bwana Paul anajiunga na klabu hiyo kwkuratibu shughuli zote za kimichezo ndani ya klabu akishirikiana kwa karibu na kocha wa klabu hiyo Eddie Howe.

Klabu ya Newcastle ambaye imemruhusu Dan Ashworth siku kadhaa nyuma kujiunga na klabu ya Man United ambapo walimchelewa sana kumuachia, Hivo hii inaleta picha kua klabu hiyo ilikua inakomaa kupata mbadala wa Ashworth ndio wamuachie kwani siku tatu nyuma wamemruhusu Ashworth na leo wanamtangaza bwana Paul Mitchell.

Acha ujumbe