Klabu ya Newcatle imetakata kwenye tuzo za mwezi ndani ya ligi kuu ya Uingereza baada ya kutoa kocha bora wa mwezi wa kumi pamoja na mchezaji bora wa mwezi huo.

Kocha Eddie Howe pamoja mshambuliaji wa klabu hiyo Miguel Almiron wamefanikiwa kubeba tuzo ya ligi kuu ya Uingereza huku kocha bora wa mwezi Howe kule mchezaji bora wa mwezi Almiron wote wakitokea klabu hiyo yenye maskani yake jijini London.newcastleHii imekuja baada ya klabu hiyo kua kwenye kiwango bora sana ndani ya mwezi wa kumi, Ikiwa wamecheza michezo mitano na kushinda minne huku wakisuluhu mchezo mmoja dhidi ya Manchester United ugenini.

Huku mshambuliaji Miguel Almiron akiwa kwenye ubora huku yeye akifunga magoli matano kwenye mitano aliyocheza ndani ya mwezi Oktoba klabuni, Hivo ni wazi kua mchezaji huyo amekua kwenye kiwango bora sana na kwa takwimu hakuna mchezaji anaemkaribia ndani ya mwezi Oktoba.newcastleKocha Eddie Howe na Miguel Almiron ni wazi kua wamestahili kubeba tuzo hizo kutokana na kua na takwimu nzuri zaidi ya wengine waliokua wanashindana nao kwa upande wa wachezaji na upande wa makocha.

Klabu ya Newcastle ni klabu ambayo imeonekana kuleta ushindani mkubwa mpaka sasa kunako ligi ya Uingereza kutokana na kiwango inachokionesha mpaka sasa, Na mpaka wakati huu wakishika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa