Klabu ya Newcastle United yathibitisha kua kiungo wake raia wa kimataifa wa Italia Sandro Tonali anachunguzwa na mamlaka nchini Italia juu ya sakata lake la kujihusisha na masuala ya kubeti.
Kiungo Sandro Tonali anayekipiga klabu ya Newcastle United mapema wiki hii alishtumiwa shirikisho la soka nchini Italia chini ya mwanasheria wa shirikisho hilo kutokana na kuhusishwa na michezo ya kubashiri.Kiungo huyo hayupo mwenyewe kwenye sakata hilo ambapo alikua na mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Italia ambaye anakipiga klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza anayefahamika kama Nicolo Zaniolo.
Klabu ya Newcastle imethibitisha uchunguzi unaendelea kwa kiungo wao huyo lakini wameahidi kumuunga mkono mchezaji huyo yeye pamoja na familia yake katika kipindi chote ambacho uchunguzi utakua unaendelea juu ya madai yake ya kujihusisha na kamari.Imekua kama utaratibu kwa wachezaji kutoka nchini Italia kujihusisha na michezo ya kamari na mara kwa mara wamekua wakifungiwa, Lakini pia haiishii kwa wachezaji mpaka timu zimekua zikihusishwa na upangaji wa matokeo kama klabu ya Juventus imewahi kuwakuta na kushushwa daraja.