Nyota wa PSG Neymar, anaripotiwa kuwa aliiomba klabu yake kuweka kipengele kwenye mkataba wake kitakacho mruhusu kuondoka klabuni hapo ikiwa Mbappe hatasaini mkataba mpya.

Neyamar alisaini mkataba mpya wa kuendelea kuwepo Parc des Princes kwa miaka minne zaidi, mwezi uliopita na kuzima tetesi nyingi juu ya hatma yake na PSG.

Hata hivyo, mwanatimu mwenzake ambaye pia ni rafiki yake mkubwa, Kylian Mbappe bado jhajasaini makubaliano mapya ya kusalia klabuni hapo. Ikiwa mbappe hatasaini mkataba mpya, basi atakuwa wakala huru msimu ujao.

Nyota huyo wa miaka 22, amekuwa akiendelea kuhusishwa zaidi na Real Madrid, lakini raisi wa PSG Nasser Al-Khelaifi amesisitiza kuwa Mbappe haendi popote.

MBappe na Neymar

Changamoto kwa PSG 

PSG iko kikaangoni kufanya maamuzi magumu. Lakini Neymar ndiye ana nafasi kubwa ya kuamua kuwapa nafuu PSG au kuwaweka kwenye kibarua kigumu.

Ikiwa Mbappe atakataa kusaini mkataba mpya, kuna hasara ya wote wawili kuondoka msimu ujao, kwa kuwa Neymar atataka kuondoka pia. Ikiwa PSG wataamua kumuuza sasa kuepuka hasara ya kumpoteza kama mchezaji huru, basi wana mfungulia mlango Neymar pia kutokana na kipengele kilichopo kwenye mkataba wake.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa