Neymar Aibua Utata Tena Brazil

Nyota wa Santos na nahodha wa Brazil, Neymar Jr., ameibua mjadala mkubwa baada ya kukosa mechi ya klabu yake ili kushiriki mashindano ya poker ya siku mbili jijini São Paulo. Hii imekuja muda mfupi baada ya Brazil kutolewa kwenye Kombe la Dunia 2026 na Norway, hali iliyompa mapumziko kadhaa kabla ya kurejea kwa hatua muhimu ya msimu.

Neymar Aibua Utata Tena Brazil

Kwa mujibu wa AS, mashabiki na wachambuzi walimkosoa vikali Neymar kwa kiwango chake kwenye Kombe la Dunia chini ya kocha Carlo Ancelotti, wakihisi hakutoa mchango uliotarajiwa. Kukosekana kwake kwenye mechi ya Santos kulionekana kama ishara ya kutojitolea, jambo lililozua hasira zaidi.

Neymar hakusita kujibu. Kupitia video aliyoposti kutoka kituo cha mazoezi cha Santos, alisema, “Nilikuwa hapa nikijiandaa kwa mazoezi ya pili, na nikakumbuka watu wengi walizungumza kuhusu mimi kucheza poker siku yangu ya mapumziko. Nilifanya mazoezi asubuhi, sikushiriki mechi, kisha nikarudi mazoezini. Ilikuwa siku yangu ya mapumziko, na bado wanazungumza.”

Neymar Aibua Utata Tena Brazil

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa bahati nzuri kwa Santos, kutokuwepo kwake hakukuathiri matokeo. Timu ilishinda kwa kishindo 4-1 dhidi ya Universidad Central de Venezuela, ikikaribia kufuzu hatua inayofuata ya Copa Sudamericana.

Neymar Aibua Utata Tena Brazil

Mashabiki sasa wanatarajia kurejea kwake wikiendi ijayo, wakati Santos watakapokutana na Chapecoense kwenye ligi ya Brazil. Swali kubwa ni kama Neymar ataweza kuondoa kelele za nje ya uwanja na kuonyesha tena kiwango cha nyota wa dunia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.