Neymar bado yupo katika sintofahamu ya hali yake ya mkataba na Paris Saint Germain, na minong’ono inataja kuwa hatarajii kuongeza mkataba mpya.

Taarifa zinasema ikiwa Neymar hatasaini mkataba mpya na PSG, basi anajiandaa kurejea Barcelona, na atakuwa tayari kukubali punguzo la mshahara wake wa sasa.

Tangia msimu uliopita mshambuliaji huyu wa PSG alikuwa akihusishwa na kurejea Barcelona, lakini maswala ya fedha yakawa magumu kukamilisha uhamisho wake kwa upande wa Barcelona.

Neymar aliripotiwa kuwa kwenye maendeleo mazuri ya mzungumzo ya mkataba wake, lakini akasitisha mazungumzo hayo. Taarifa zinasema kuwa alipewa mda wa kukamilisha suala hilo, akihitajika kusaini kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Kwa mujibu wa Marca, Neymar atakuwa tayari kupunguziwa mshahara ili arejee Barcelona ikiwa hatasaini mkataba mpya na PSG wa kuendelea kuwepo zaidi ya msimu wa 2022.

Nyota huyu wa zamani wa Barcelona, mara nyingi amekuwa akizungumzia nia yake ya kuungana tena na Lionel Messi. Messi pia alikuwa akihusishwa na PSG, ikiwa Messi anasalia Barcelona, basi huu unaweza kuwa wakati muafaka.


 

MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

Neymar, Neymar Atakubali Kupunguziwa Mshahara?, Meridianbet

CHEZA HAPA

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa