Neymar Atemwa na PSG Kuuanza Msimu Ligue 1

Staa wa Brazili na PSG, Neymar Jr ametemwa nje ya kikosi kinachoenda kuufungua msimu wa Ligue 1. Taarifa zinazobamba zaidi ni kuhusu uwezekano wa nyota huyu kusalia klabuni hapo au kuondoka kutokana na hali iliyopo sasa.

Baadhi ya vyanzo vinataja kuwa klabu ya PSG ipo mbioni kufanya maamuzi juu ya uhamisho wa staa huyu. Hvyo kwa mujibu wa vyanzo hivi hatma ya Neymar itafahamika punde tu wakuu wa klabu hii wakiafikiana.

Kufuatia Neymar kuachwa kwenye kikosi cha PSG kinachotarajiwa kucheza na Nimes, kocha wa klabu hii, Thomas Tuchel amedai kuwa ni kwa sababu staa huyu hakuweza kumaliza wiki ya mazoezi na timu hiyo.

Neymar Atemwa na PSG Kuuanza Msimu Ligue 1
Real Madrid wanatajwa kuwa wnajaribu kumsajili nyota huyu wakati Barcelona wakiwa karibu pia.

Chanzo kingine kutoka klabu hiyo kilinukuliwa kikisema Neymar hana shida yeyote ya Afya, yuko sawa isipokuwa wapo katika hatua za maamuzi juu ya hatma yake.

Neymar alijiunga na PSG akitokea Barcelona mwaka 2017, kwenye dili lililokuwa na thamani ya paundi milioni 222. Hakuwa na kipindi kizuri sana PSG baada ya kuandamwa na majeraha. Mkurugenzi wa michezo wa PSG, Leornando Araujo alisema kuwa staa huyu ataondoka klabuni hapo akipatikana mnunuaji. Klabu za Real Madrid na Barcelona zinahusishwa na kuwinda sahihi yake.

Acha ujumbe