Staa wa timu ya taifa ya Brazil Neymar Jr amesema gwiji wa soka wa nchi hiyo Pele amefanikiwa kuugeuza mchezo wa mpira wa miguu kua mchezo wenye hadhi ulimwenguni.
Mchezaji huyo wakati akitoa salamu za pole baada ya gwiji Pele kufariki dunia siku ya jana na mchezaji huyo kusema Pele alibadilisha taswira ya mchezo wa mpira wa miguu milele, Gwiji huyo aliaga dunia baada ya kusumbuliwa na saratni ya utumbo kwa muda mrefu.
Neymar aliandika kwenye mitandao yake ya kijamii kua kabla ya Pele mchezo wa mpira wa miguu ulikua mchezo wa kawaida tu, Lakini gwiji huyo alibadilisha kila kitu kwani alifanikiwa kubadilisha mpira wa miguu kua sanaa, Burudani, Sauti kwa watu wa hali ya chini, Lakini pia aliitambulisha Brazil duniani kote.
Mchezaji huyo ambaye aliendelea kuonesha huzuni yake baada ya Pele kufariki na kuendelea kumimina sifa kwa gwiji huyo na kusema hata jezi nambari kumi kwenye mpira wa miguu ilikua jezi ya kawaida, Lakini ilipata heshima na hadhi baada ya kuvaliwa na gwiji huyo.
Mchezaji Neymar ambaye alifanikiwa kufikia rekodi ya mabao ya gwiji Pele ya magoli 77 kwenye timu ya taifa ya Brazil kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar, Alisema gwiji huyo ameondoka lakini ameacha alama kubwa kwenye mpira na maajabu yake yataishi milele.


