Neymar Tena!

Ikiwa zimebaki siku kadhaa tu timu za bara la Amerika zianze kuumiza nyasi kuna balaa limeanza kukikumba kikosi cha Tite huku wachezaji wa kutegemewa ndani ya kikosi hicho wakianza tayari kupata majeraha jambo ambalo linaanza kuwatia wasiwasi mapema sana mashabiki wa kikosi hicho.

Brazil ni miongoni mwa timu zinazotabiriwa kuwa na ushindani wa kipekee ndani ya mashindano hayo, jambo ambalo kwa hakika sio la mchezo kwa timu hiyo ambayo inategemea kwa kiwango kikubwa wachezaji wa aina yake ili kuweza kufikia malengo makubwa na ya pekee sana ya kikosi hicho.

Neymar akiwa ameitwa kuweza kushirikiana na wachezaji wengine ndani ya kikosi hicho amepata majeraha ya goti ikiwa ni tatizo lake la muda mrefu na ametonesha tena eneo hilo la mwili wake kwa mara nyingine na hii inaweza kuwa sio dalili nzuri nzuri kwake.

Baadhi ya vyombo vya habari vilivyokuwa jirani na eneo hilo la mazoezi vinaripoti kwamba nyota huyo alionekana akishika eneo hilo la mguu wakati wakiwa mazoezini na jopo la madaktari lilionekana kumuangalia kwa karibu lakini baadaye iliripotiwa kwamba amepata majeraha katika eneo hilo.

Tatizo hilo linakikuta kikosi hicho zikiwa zimesalia siku 16 pekee ili harakati hizo zianze kutimua vumbi ndani ya taifa hilo la Brazil ikiwa linafanyika nchini humo tangu lilipofanyika kwa mara ya mwisho mwaka 1989. Watakuwa wenyeji wa kombe hilo ndani ya mwaka huu wa kimashindano.

Wenyeji hao wataanza kampeni dhidi ya Bolivia na kufuatiwa na Peru ambao mara nyingi hushindana nao kutokana na upinzani mkubwa wanaouonesha mara wanapokutana. Na kama inavyofahamika kwamba ndani ya bara hilo kuna ushindani mkubwa sana na kuna wachezaji wenye viwango na uwezo mkubwa sana.

Hilo linatokea huku timu hiyo ikiwa tayari imempa kitambaa cha unahodha mchezaji huyo ili aweze kuongoza kikosi hicho mara baada ya kutokea sintofahamu kwa mkongwe wao waliyekuwa naye ambaye ni Dani Alves. Hivyo, basi kutakuwa na kila linalowezekana ili aweze kufanya vyema kama akirejea kwenye nafasi hiyo.

Mapema mwezi uliopita aliwekwa nje ya uwanja kutokana na adhabu aliyokuwa akiitumikia baada ya kutumia lugha isiyo ya kiuungwana akiwa jukwaani mara baada ya kutolewa nje ya michezo ya klabu bingwa Ulaya na Manchester United hivyo hajapata muda wa kutosha kuweza kukaa uwanjani.

4 Komentara

    pole kwa neymar na kikosi chaka

    Jibu

    Noma sana

    Jibu

    Pole sana neymar

    Jibu

    Pole sana mpambanaji neymar

    Jibu

Acha ujumbe