Ngolo Kante aliamua kuiacha Mini Copper yake nyumbani akaamua kuchukua treni wakati akiripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya EURO juzi.

Kwa bahati mbaya treni ilichelewa kwasababu ya hitilafu iliyotokea katika kituo kimoja. Ngolo Kante akachelewa kuripoti kambini.

Alipofika kambini, kikao kilishakwisha na wachezaji walikuwa wanaendelea na mambo mengine.

Ngolo Kante
Kante

Alifika kwa kocha Didier Deschamps na kumpa tabasamu kama kawaida yake kisha akamuambia nimecheleweshwa na treni.

Didier Deschamps hakuwa mkali kwake. ‘Anajua tu huyu ni Ngolo Kante na hawezi kuchelewa nje ya taratibu kwasababu za kihuni’.

Didier Deschamps alimpa tabasamu na kumuambia, “Lakini Ngolo upo fasta kuliko treni kwanini hukuiacha kisha ukaja mwenyewe??” . Walicheka wote kisha kesi iliishia hapo.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa