Usiku wa leo kutakua na mchezo mkali wa kukata na shoka wa ligi ya mabingwa ulaya ambapo klabu ya Inter Milan itakua nyumbani kuikaribisha miamba ya soka kutoka nchini Hispania klabu ya Atletico Madrid.
Inter Milan wanafainali hawa wa ligi ya mabingwa barani ulaya msimu uliomalizika wakiwa vinara wa ligi kuu ya nchini Italia Serie A watakua ni kibarua cha kumenyana na klabu ya Atletico Madrid vijana wa kocha Diego Simeone ambao wako kwenye kiwango bora pia msimu huu.Vilabu hivi vinakutana katika hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa ulaya kila mmoja akitafuta tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, Huku mchezo ukitarajiwa kua mkali kutokana na ubora wa vilabu vyote viwili.
Vinara hao wa ligi kuu ya Italia wamekua na msimu bora sana mpaka wakati huu na kua moja ya timu ambazo zinapewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo msimu huu,Kama wakifanya vizuri itakua ni mara ya pili mfululizo kwani msimu uliomalizika walikua wanafainali wa michuano.Klabu ya Atletico Madrid wao wanaingia kwenye mchezo huu bila unyonge kwani klabu hiyo kutoka nchini Hispania wana ubora vilevile, Hivo wana uwezo wa kufanya chochote katika mchezo wa leo licha ya Inter Milan kuonekana kupewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda mchezo.