Ni Messi au Rashford?

Leo historia inajengwa ndani ya uwanja wenye historia ya kufanya makubwa kwenye maisha ya soka. Ni pale ambapo miamba wawili wa soka wenye historia nzuri ya vikombe na kuwa na majina makubwa yaliyojengwa kutokana na uwezo wao watakapotoana jasho kuwania nafasi ya kuelekea nusu fainali ya ligi ya mabingwa.

Masikioni mwa watu wengi wanaopenda kuona soka bora ni je, Messi ataenda kuwafanya nini Manchester ambao hawajawa na msimu mzuri sana wa kujisifu kwamba wamefanya mambo ya pekee ili kudhihirisha ubora wao kuondoka na ushindi mbele ya ardhi hiyo na huku wakiendelea kupata majeruhi wa kikosi chao cha kwanza.

Kocha mpya wa klabu hiyo, Ole Gunnar ana kazi ya pekee kuuaminisha ulimwengu wa wanasoka kama kikosi chake kina uwezo wa kupambana na Barcelona ambao kwa msimu huu wamekuwa na mwenendo unaoeleweka hata ndani ya ligi yao ya Hispania na vikombe vingine nje ya ligi ambavyo ameshiriki.

Sio jambo dogo kuzuia baadhi ya wachezaji kufanya yale wanayoweza kuyafanya uwanjani baadhi yao ni Messi ambaye mara nyingi ndiye mwokozi wa jahazi la klabu hiyo ya Barcelona na huipa matokeo hata wakati mgumu ambao klabu inaonekana kuelemewa. Hivyo, United wana kazi kubwa sana kuzuia safari ya mchezajj huyo.

Kwa kikosi kazi cha United kwa sasa wana la ziada la kufanya ili kuhakikisha wanamdhibiti Messi asitembee ili kuleta madhara kwenye safu yao lakini wakati wanamdhibiti kuna nyota wengine hatari kama Suarez, Coutinho watakuwa na upenyo wa kufanya yao kutokana na kuzuiwa kwa nyota huyo kusafiri na mpira.

Lakini pia upande wa pili, United naye akiweza kuhimili kasi ya viungo wa Barcelona kama Rakitic na Sergi basi wataweza kushambulia kwa namna wanayotaka wao na wanayoona wao ni sahihi maana uwepo wa watu kama Rashford hawezi kuwapa uhuru mabeki kama Lenglet na Pique kusafiri wanavyotaka kutokana na kasi ya nyota huyo.

Kuelekea mechi yao, United bado atakuwa na upungufu wa wachezaji wake wa kikosi cha kwanza kama Herrera, Vakencia, Baily na Matic ambao hawakuonekana kabisa mazoezini wakiwa na timu yao. Lakini wamepata nafasi ya kurudi kwa nyota wao wengine kama Sanchez na Rashford aliyekuwa na majeraha kidogo.

Lakini upande wa Barcelona mara nyingi wao huhofia utimamu wa mwili wa Messi kuliko wachezaji wengine kutokana na ule msemo usemao yeye ni mbadili matokeo ya mchezo wakati wowote na akiwa imara yeye jambo hilo huwa haliwaumizi kichwa kabisa. Lakini mbali na hao ambao afya zao zinawaruhusu kushiriki mechi ya leo wapo wengine ambao watakuwa nje ya kikosi kama Rafinha na hali ya Dembele ni mguu nje mguu ndani kama anaweza akacheza au akapumzishwa.

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa