Mara nyingi nimekuwa nikiandika soka ni taaluma kamili ambayo inahitaji kujitoa sana ili kuwa vyema na taaluma hiyo kama zilivyo taaluma zingine; udaktari, udereva, ukutubi, uhasibu na zinginezo.
Timu ya mpira wa miguu yenye wachezaji 11 uwanjani imegawanyika katika sehemu kuu tatu ; safu ya ulinzi , kiungo na ushambuliaji. Mgawanyiko huu kiuchezaji hujengwa katika sehemu kuu tatu ; sehemu ya kwanza ni umbo la uchezaji ( tactical formation) . Sehemu ya pili ni mbinu za uchezaji katika mfumo husika ( defensive and offensive technical patterns) na mwisho ni eneo muhimu sana la saikolojia ambalo huanzia nje ya uwanja kuja ndani. Hili liko katika mental analysis. Uwezo wa waalimu na uongozi kuweka msukumo wa ndani kwa timu na mchezaji mmoja mmoja kucheza kwa moyo wote kuipambania timu.
Sasa katika mgawanyiko huo; katika kila idara mwalimu au kocha huwa na key player wa kuleta matokeo chanya kwa timu au wenzake. Kwa mtazamo wa nje , mimi na wewe tunaweza tusimuelewe mwalimu au uongozi kumng’aninia mchezaji fulani lakini kumbe kwao ni lulu inayotunzwa iletayo matokea chanya indirectly.
Si kila mchezaji anaweza kukupa positive impacts kwenye patterns zote, yaani awe bora katika kulinda timu na kushambulia pia awe na saikolojia nzuri. Akitokea wa hivyo huitwa kiraka (versatile).
Carlos huyu mimi namuita ni mchezaji wa kuamua timu ishambulie vipi au ipate matokeo kwa njia gani. Ni aina ya wachezaji ambao wanampa mwalimu msingi plan B zao katika kuamua matokeo. Si aina ya mchezaji ambaye utamtegemea kwenye marking au kufanya pressing kwa ukokotaji, ila ni aina ya wachezaji ambao mpira ukiwa mguuni kwake unaanza kujipa asilimia kubwa ya kukuinua katika mfumo na mbinu zako za kutafuta goli. Hivyo katika ule mgawanyiko pale juu, huyu anaingia katika mnyumbuliko (flexibility) ya offensive patterns katika plan A au B za kutafuta matokeo.
Sven kocha mkuu wa Simba SC ni nadra sana kukuta anamuongelea mchezaji mmoja kwa matokeo ya timu lakini muda mwingi hushindwa kuzuia hisia zake kwa Luis Misquissone . Ni kiumbe ambaye kwa sasa pale Simba ndio anaubeba mfumo wake A na B wa kushambulia.
Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!
Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!
Issa
Carinhos mguu wa dhahabu akipiga mpira atakapo ndipo utafika yah yupo carinhos mmja tu
Hopemwaikuka
Mmh
Amiri Kayera
Me naona km kocha anashindwa kumtumia vizur
Theckla
Mda bado
Dorophina
Carinhos yupo vizuri sana
Sauda
Carinhos anajituma.
Venerose
Duuh
magdalena
kocha anabidi amtumie vizuri sana uyu kijana atawaonesha maajabu mengi
Zeiyana
Yupo vizuri sana akiwa kwenye imaya yake carinhos
Lydia Emmanuel Magoti
Yupo vizuri Dogo ila kocha Kama atomtumia vizuri atazidi kulala Dogo huyo mwenendo wake upo vizuri Ila wanabugi kwake wampange kisawa sawa Dogo atulie huyo anajua
Caroline
Carlinho ni levels..
Nasra
Yupo vzuri sana
Tatu
Kocha wa yanga bado awajawandaa wachezaji wake vizuri na kuwaelewa ingawa wanawachezaji wazuri sana
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
Ester mmakasa
Ni kweli kabisa
Angelina
Hana maajabu
Shani
Muda utaongea utamfaham tu
Gabriel
kocha anashindwa kumtumia vizur
Rose kapinga
Yanga ni carilnhos tuu wengine tupa kule mnampa kazi ngumu mtoto wa watu ya kubeba timu yote
lombo
duh
Sabrina
Muda bado mtamuelewa tu
felister
kweli kabisa
Saupha mohamed
Duuuh
Mwajumah
Yupo vizuri sana
Fatina mfigi
Mmmh
aisha
Yuko vizuri sana
David Pere
Carlos huyu mimi namuita ni mchezaji wa kuamua timu ishambulie vipi au ipate matokeo kwa njia gani. Ni aina ya wachezaji ambao wanampa mwalimu msingi plan B zao katika kuamua matokeo. Si aina ya mchezaji ambaye utamtegemea kwenye marking au kufanya pressing kwa ukokotaji, ila ni aina ya wachezaji ambao mpira ukiwa mguuni kwake unaanza kujipa asilimia kubwa ya kukuinua katika mfumo na mbinu zako za kutafuta goli. Hivyo katika ule mgawanyiko pale juu, huyu anaingia katika mnyumbuliko (flexibility) ya offensive patterns katika plan A au B za kutafuta matokeo.