Hapa Ronaldo kule Salah hapatoshiii!! Man Utd watamenyana na Liverpool leo Usiku huku kikosi cha Erik ten Hag kikiwa mwishoni mwa msimamo wa ligi, Liverpool iliifunga United 9-0 kwa jumla ya mechi mbili za ligi msimu uliopita.

ronaldo,Salah, Ni Ronaldo au Salah Kung’ara Usiku wa Leo?, Meridianbet

Chini ya msimamo, bila alama, inafikirisha sana kuhusu kikosi cha Man United chini ya kocha wao mpya ambaye bado hajatulia katika klabu hiyo. Inawezekana pambano la Usiku wa leo dhidi ya Liverpool halionekani kuwa zuri kwa Manchester United.

Baada ya kushindwa na Brighton na Brentford katika mechi zao mbili za mwanzo za msimu huu, kikosi cha Erik ten Hag kinapata shida sana haswa kwenye safu yao ya ulinzi inapokutana na timu yenye washambuliaji bora wanaofika kwenye goli la mpinzani, lakini katika mechi ya leo kocha mkuu wa Man United, ana jambo la kufanya ili kupunguza machungu kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kichapo kwenye mechi mbili za mwanzo wa ligi.

Ronaldo

Lakini wachambuzi wengi wa soka wamezungumzia  kiwango cha United kwa hivi karibuni, pia kuna hoja nyingine  inakuja katika mfumo wa Liverpool kuangusha alama zaidi nyumbani dhidi ya Crystal Palace.

Ghafla, vijana wa Jurgen Klopp wameshindwa kupata ushindi katika mechi zao mbili za mwanzo pia endapo Man United itapata ushindi hii leo hautapunguza tu baadhi ya matatizo lakini pia utawaweka juu ya wapinzani wao wakali kwenye msimamo.

Je ni Timu Gani Itaondoka na Alama Zote 3 Leo?

Liverpool kupoteza pointi mara kwa mara mapema katika msimu inaweza kuonekana ajabu kwa wengi, lakini ukirejea nyuma katika msimu uliopita unaweza kuwa sawa na jinsi walivyouanza msimu hu una kampeni yao ya kusaka ubingwa.

Katika mechi zao tisa za mwisho katika michuano yote bila kujumuisha ushindi wa Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester City, katika mechi za kujiandaa na msimu mpya Liverpool wameruhusu bao la kwanza katika mechi nane kati ya hizo nane, isipokuwa ni fainali ya Kombe la FA isiyo na mabao dhidi ya Chelsea, ambayo walilazimika kushinda kwa mikwaju ya penalti.

ronaldo,Salah, Ni Ronaldo au Salah Kung’ara Usiku wa Leo?, Meridianbet

Kwa ufupi, Liverpool wana tabia ya kuanza ligi kwa mwendo wa kobe, Kila moja ya mechi tisa zilizopita imekuwa na mwelekeo tofauti, wameruhusu goli katika dakika 15 za kwanza katika mechi nne kati ya tisa za mwisho.

Liverpool Bado Atawakosa Baadhi ya Wachezaji Wake Muhimu Kwenye Mchezo wa Leo.

Kwa upande wa Man UTD mengi yamefanywa kuhusu kuongeza ari ya upambanaji katika kambi ya United katika kipindi cha wiki mbili zilizopita. Lakini hali sio nzuri sana kwa Liverpool, haswa linapokuja suala la majeraha kwa wachezaji wao tegemezi.

“Ilikuwa kama tulikuwa na mchawi ndani ya kambi,” alisema Klopp, ambaye anapitia changamoto ya majeruhi kwa wachezaji wake.

Wasiwasi mkubwa wa Liverpool ni katika safu ya kiungo, huku Thiago Alcantara akiwa nje kwa mwezi mmoja, na Curtis Jones na Alex Oxlade-Chamberlain pia wanaendelea kutibiwa. Hilo linawaacha Jordan Henderson, Harvey Elliott na James Milner kumsaidia Fabinho ili kuongeza nguvu katikati ya uwanja, huku Naby Keita akionekana kutofurahishwa na kukosa muda wa kucheza Liverpool.

ronaldo,Salah, Ni Ronaldo au Salah Kung’ara Usiku wa Leo?, Meridianbet

Wakati huohuo, Joel Matip ana mapungufu kwenye safu ya ulinzi hivyo Nat Phillips na Joe Gomez watachuana kuwania nafasi ya kucheza na Virgil van Dijk katika safu ya ulinzi wa kati, huku kukiwa na upungufu mkubwa wa mshambuliaji kwani Darwin Nunez ana kadi nyekundu aliyopata dhidi ya Crystal Palace, Diogo Jota bado ni majeruhi na Roberto Firmino amerejea tu kutoka kwenye majeraha na hayuko vizuri kwa asilimia 100.

Ingawa Liverpool wanakabiliwa na majeraha na wasiwasi mdogo juu ya kushinda leo, bado wana chaguo la kwanza kutoka kwa Mohamed Salah.

ronaldo,Salah, Ni Ronaldo au Salah Kung’ara Usiku wa Leo?, Meridianbet

Msimu uliopita, winga huyo wa Misri aliisababishia United matatizo chungu nzima, akifunga mabao matano na kutoa pasi mbili za mabao katika michezo hiyo miwili, ambayo Liverpool walishinda kwa jumla ya mabao 9-0.

Hivyo basi Salah ana mzigo mkubwa wa kuibeba mabegani mwake timu yake huku kwa upande wa Man UTD wakimtegemea Zaidi mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo kuwapatia ushindi muhimu kwenye mechi ya leo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa