Ni Wakati Sahihi?

MSIMU ujao klabu ya Chelsea itakuwa ikiwakilisha Uingereza kwenye michuano ya kimataifa hususan klabu bingwa na kwa sasa wanashikilia rekodi ya kunyanyua kombe la Europa League baada ya kuwashinda washindani wao Arsenal msimu uliopita.

Baada ya mafanikio hayo, Chelsea walionekana kuanza kuangalia kocha mwingine wa kumpa mkataba wa kudumu kukinoa kikosi chao mbali na Sarri ambaye alipokea kibarua cha haraka baada ya Conte kushindwana na uongozi wa juu wa klabu hiyo. Hivyo, kufikia maamuzi ya kuangalia ambaye angeweza kusukuma kikosi kwa wakati ule.

Klabu nyingi duniani huamini wachezaji ambao kwa namna fulani huwa wamewapa msingi fulani na wanaijua falsafa ya klabu yao kwa namna ya pekee sana. Hata wanapowapa nafasi wachezaji hao, hasa zile za kuviongoza vikosi vyao hivyo huamini kwamba watakuwa na damu halisi za pale ambapo pamewatoa.

Katika kuamini hilo, klabu ya Chelsea inaonekana kuanza mipango ya kumshawishi Frank Lampard kukaa na kikosi chao hicho ili kusonga nacho mbele msimu ujao. Hilo linatokana na imani kubwa iliyojengwa kwake kihistoria tangu alipoichezea klabu hiyo kwa kipindi chote.

Msimu huu alifanya vizuri sana na klabu ya Derby ambayo ilikuwa ikipigania nafasi ya kupanda ligi hiyo japo bahati haikuwa kwao na kumuachia mchezaji mwenzake, John Terry ambaye amecheza naye ndani ya ligi hiyo lakini wakiwa wanafundisha klabu mbili tofauti akaipandisha Aston Villa kwenye ligi.

Amehusishwa kwenye nafasi hiyo akiwa na majina ya makocha wengine kama Nuno Espirito Santo, Javi Gracia, Massimiliano Allegri na Erik ten Hag ambao wanahusishwa kuifundisha klabu hiyo lakini hadi sasa mchezaji huyo wa zamani wa klabu hiyo anaonekana kupigiwa upatu sana kujiunga kuwanoa mabingwa hao.

Sarri anayetegemewa kuondoka klabuni hapo kwa sasa anahusishwa na kuinoa klabu ya Juventus huku akiwa anapigiwa upatu na wachezaji wengi kwamba ni kocha sahihi kwa mfumo wa klabu hiyo na ataweza kuipa mataji zaidi kama akipewa nafasi.

Je, huu ni wakati sahihi kwa Lampard kukabidhiwa kikosi hicho?

Ngoja tuwe na subira kuona kama ataweza kukifikisha kikosi hicho kwenye malengo yake.

2 Komentara

    Vizur

    Jibu

    Ngotuone kwanza

    Jibu

Acha ujumbe