Ripoti zinazidi kubamba huko Uhispania na Italia kwamba Atletico Madrid wanamwona mshambuliaji wa Napoli Arkadiusz Milik kama mbadala mzuri wa Diego Costa.
Inadaiwa Costa anataka kusitishwa kwa mkataba hapo Januari kwa makubaliano ya pande zote ili aweze kurejea Amerika ya Kusini kwa sababu zake binafsi.
Milik anazidi kuonekana kama chaguo la kwanza kama mbadala wake, na kwa mujibu wa vyanzo vya AS, Mundo Deportivo na Marca, vyote vinamtaja mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland kuingia kwenye malengo ya Atletico.

Milik hajapata fursa ya kucheza kuichezea Napoli msimu huu baada ya kuachwa kikosini tangia alipokataa kusaini mkataba mpya au kukamilisha uhamisho wa kuhamia kwenda Roma.
Mkataba wake wa sasa na Napoli unamalizika mwezi Juni 2021 na hiyo inatajwa kuwa inaweza kuwa changamoto katika kukamilisha uhamisho wake kwenda Atletico, kwa kuwa anaweza kulazimika kusubiri miezi sita zaidi ili aweze kuwa mchezaji huru na kusajiliwa bure msimu ujao.
Napoli wanahitaji angalau €15m kuachana na mshambuliaji huyu, pungufu ya dau la awali la €18m waliyokuwa wanaihitaji msimu wa joto.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?
Issa
Simeon kocha mwny ubunifu
warda
Mbona Diego anafanya poa tu
Tatu
Mbona mapema Napoli kumuachia milk
Fatina mfingi
Mmmh
Mwanahamisi
Diego Yuko poa
Sarah
Yuko poa sana Diego
Rahmal
Diego Yuko vizuli
Hopemwaikuka
Anafaa sana
Saupha mohamed
Diego namkubali
Angelina
Dieogo yuko vizuri
Dorophina
Milik akienda atletico itakuwa poa sana
Zahara omary
Dieogo yuko vizur snaa
Lydia Emmanuel Magoti
Diego yupo vizuri anajua
Sania
Diego jembe