Baada ya kuhusishwa na vilabu mbalimbali bila mafanikio, hatimaye beki wa Ajax Amsterdam – Nicolas Tagliafico ameamua kubaki Uholanzi mpaka 2023.

Hatua hii inafikiwa baada ya wakala wa Nicolas Tagliafico kuthibitisha mchezaji huyo atasaini mkataba mpya utakaomfanya aendelee kuwepo klabuni hapo kwa muda wa mwaka mmoja zaidi.

Mkataba wa sasa wa Tagliafico unamalizika 2022 na kwa hatua hii, ni dhahiri mchezaji huyo raia wa Argentina ataendelea kuwepo Ajax mpaka mwisho mwa msimu huu.

Nicolas Tagliafico, Nicolas Tagliafico Kubaki Ajax Mpaka 2023., Meridianbet
Nicolas Tagliafico

Hii ni habari mbaya kwa vilabu ambavyo vilikuwa vinaiwania saini ya beki huyu ambaye ameshapachika magoli 16 tangu 2018. Katika dirisha la usajili lililopita, Ajax walihitaji kiasi cha pauni milioni 20 ili kumuachia Tagliafico, dau ambalo hakuna timu ilikuwa tayari kulitoa kutokana na kuporomoka kwa uchumi kwenye vilabu vingi.

Inasemakana, moja kati ya makubaliano yaliyopo kwenye mkataba mpya wa Nicolas Tagliafico ni kumaliza msimu huu akiwa na Ajax na kuanzia msimu ujao ataruhusiwa kujiunga na timu yeyote kwa dau ambalo bado halijawekwa wazi.

Chelsea na Manchester City ni miongoni mwa vilabu vilivyokuwa vinaiwinda saini ya Tagliafico na sasa wataendelea kusubiri kwa muda mrefu zaidi kama bado wataendelea kumuhitaji mchezaji huyo.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

17 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa