Nikimuangalia Bale Namkumbuka Winston Bogarde

Rafiki yangu mmoja alinipigia simu kuniuliza maoni yangu juu ya Gareth Bale. Kwanini hataki kuondoka Real Madrid wakati ameshaambiwa kuwa hatakiwi na hayupo kwenye mipango? nilimpa jibu jepesi tu, ‘PESA’. Sijui kama alinielewa. Ila hiyo ndiyo sababu. PESA tu! Hakuna kingine.

Basi wakati namuelezea kwanini pesa ndio inamuweka Gareth Bale Madrid, kichwani mwangu akanijia mtu aliyeitwa Winston Bogarde. Beki wa kiholanzi aliyesajiliwa na Chelsea mwaka 2000. Alisajiliwa akitokea Barcelona akiwa na miaka 29 tu na kocha Gianluca Viali. Alisaini kandarasi itakayompatia mshahara wa paundi arobaini elfu kwa wiki.

Hii pesa ni nyingi sana. Mateo Guendouzi kwa sasa anatamba pale London kwa mshahara kama huo. Fikiria miaka 20 iliyopita ilikuwaje. Ilikuwa nyingi zaidi. Basi Bogarde akasaini mkataba wa miaka minne na Chelsea. Haukupita muda Vialli akafukuzwa, akaletwa Claudio Ranieri.

Ranieri hakumtaka Bogarde, akashauri auzwe. Chelsea ilimtafutia timu, ila hawakufanikiwa kwasababu ya mshahara wake. Hakuwa tayari kupunguza mshahara ili apate timu. Hakuwa tayari kuondoka kwa mkopo. Chelsea wakamshusha afanye mazoezi na timu ya watoto. Bogarde hakujali, yeye alichowaza ni pesa tu aliyokuwa anapatiwa.

Alimaliza mkataba wake na Chelsea mwaka 2004 akiwa amecheza mechi tisa tu. Akaamua kustaafu na kwenda Marekani kula pesa aliyoivuna Chelsea kwa miaka minne. Hata hivo, maisha yanahitaji nini tena zaidi ya pesa? Sidhani kama lipo jibu. Bogarde alijua hili, ndio maana hakuchezea nafasi aliyopata ya kuchuma noti.

Basi mawazo kama haya anaishi nayo binadamu aitwaye Gareth Frank Bale. Analipwa kuliko mchezaji yoyote yule Real Madrid. Sasa hawamtaki na wamemuambia wazi, ila yeye hajali. Anachojali ni kuona paundi 350,000 zikiingia kwenye account kila wiki. Maisha yanataka nini tena?

Kama ni mataji ameshanyanyua ya kutosha. La Liga, Copa del rey, UEFA. Anataka nini tena zaidi ya pesa? Anajua kwa umri na uwezo wake hawezi kupata timu itakayomlipa ‘kibingwa’ kama wanavomlipa Real Madrid kwa sasa. Kumbuka Bruno Fernandes anakula paundi laki moja kwa wiki. Sasa kwanini Gareth Bale aondoke? Tumuache apige pesa.


Beti Mbio za Mbwa Mubashara

Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.

Cheza Hapa

47 Komentara

    Bale amenifurahisha sana nadhani Binafsi ana cha kupoteza ila anataka kuikomoa Madrid na Zidane

    Jibu

    bale yupo vizuri sana na navyoona sidhani kama ana mpinzani

    Jibu

    Bale hana Cha kupoteza ila anataka kuikomoa Madrid na Zidane tu kwa ninavyoona binafsi#Meridianbettz

    Jibu

    Jamaa yupo vizuri sana

    Jibu

    Ajawahi kukosea bale

    Jibu

    Safari ya bale inafurahisha sana real madrid kwa mimi naona kama atamaliza na nao real madrid arudi nyumbani ili kuongeza chachu ya ushindani so naona arudi tottenham

    Jibu

    Haaa Bale nimekupenda bure

    Jibu

    Bale good 👍@meridianbettz

    Jibu

    Yupo sahii Bale nimemkubali jembe Hilo lakujiamin

    Jibu

    Bale Yuko poa

    Jibu

    Bale namkubali sana yupo vizuri

    Jibu

    Bale Yuko fresh tu

    Jibu

    bale yupo vizuli sana#meridianbettz

    Jibu

    Mwisho wa siku kiendacho mfukoni ndo cha msingi

    Jibu

    Bale natumain msimu huuu unawez hukawah mwisho wake pale santiago bernabue kikubw kinachomwek pale ni pesa tu hakun kngne natumain mkataba ukifikah tamati atatafuta timu ya kucheza leo

    Jibu

    Bale namkubalii

    Jibu

    Bale hana mpinzani

    Jibu

    Bale ni mchezaji mzuri sana sema madrid hawataki kumpa nafasi ila cha kupoteza hana kabisa

    Jibu

    Nadhani mshahara anaolipwa pale madrid hata asipocheza yeye kwake poa tu.

    Jibu

    Bale yuko vzur sana namkubal Ingawa zipo klabu zinazomhemea, sioni kikosi chochote kati ya hivyo vinavyowania maarifa yake kinachoweza kumudu bei yake. Ni pigo kubwa sana kwamba kwa sasa hajakuwa akiunga kikosi cha kwanza cha Real. Licha ya kuhangaishwa huko, hatahiari kuondoka akasema Barnett.
    Kufikia sasa, Bale anajivunia kufungia Real zaidi ya mabao 100 na kushindia miamba hao wa soka ya Uhispania mataji manne ya La Liga nkubal sana huyu jamaa

    Jibu

    Namkubar Sana Bale

    Jibu

    Bale yuko pouwa

    Jibu

    Licha ya kuambiwa kwamba hayupo kwenye mipango ya zidane ila bale anaangalia pesa clubuni hapo anazolipwa.

    Jibu

    Duu pesa si mchezo ata akae benchi kwa kiasi gan pesa tuu ndio ilitawala kichwan kwake

    Jibu

    Bale nais amelizk maish ya pale

    Jibu

    Bale yupo vzr

    Jibu

    Daah wameshamchoka sasa.

    Jibu

    Bale nmekukubali mwanang umetishaa n hyo ndo akili sasa

    Jibu

    Mwache ale pesa zake bale

    Jibu

    Asante kwataharifa

    Jibu

    Sio yeye tu hata Wayne Bridge alifanya hivyo akiwa Man City na Chelsea na hakujali#meridianbettz

    Jibu

    Bale yupo vizuri sana

    Jibu

    Asante meridianbet kwa makala bomba

    Jibu

    Jamaa mzuri sana

    Jibu

    Piga pesa bale

    Jibu

    Bale Kama bale wakuachee!!

    Jibu

    Bale nahisi yeye nikama mwanafuzi ambae hataki shule lakini ameingia kwenye mtihani wewe unafikiri atajaza nini ndiyo bale hapendi kwenda klabu nyingine kwa sababu anataka kupata hela hiyo mana ni nyingi sana ila kama real Madrid wasipo muongezea mkataba basis mkataba wake ukiisha atakuwa mchezaji huru ila itakuwa amewanyoosha real

    Jibu

    Mimi nadhani kikubwa mkono umeenda kinywani

    Jibu

    Bale yupo vizuri

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Kwa maelezo hayo bale yupo sahihi sana ni kweli pesa ndio kila kitu katika maisha haya ya sasa na ukiangalia bale yupo vizuri sana na kama akimua kwenda clabu yoyote hanakubaliwa

    Jibu

    Bora abaki bwana

    Jibu

    Safari ya bale inafurahisha sana real madrid kwa mimi naona kama atamaliza na nao real madrid arudi nyumbani ili kuongeza chachu ya ushindani so naona arudi tottenham

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.