Miamba wa Serie A Juventus wanatajwa kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Gabriel Martinelli msimu huu wa joto.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amekuwa katika kikosi cha kwanza chini ya kocha mkuu Mikel Arteta, akifunga mabao sita na kutoa asisti saba kwenye mechi 36 kwenye mashindano yote msimu wa 2021-22.
Martinelli anaonekana kuendelea kuwa mtu muhimu kwenye mipango ya Arteta huku nyota huyo wa kimataifa wa Brazil akikabidhiwa jezi namba 11 kwa ajili ya msimu ujao.
Licha ya hayo, kwa mujibu wa Calciomercato, Juventus wamemtupia jicho Martinelli kama mchezaji wanayehitaji huduma yake wakitaka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji baada ya kuondoka kwa Paulo Dybala.
Ripoti hiyo inaongeza kuwa Juve watakuwa tayari kufanya biashara ya kubadilishana na kiungo Arthur na Martinelli, wakati miamba hao wa Italia pia wakivutiwa na wachezaji wawili wa Arsenal Gabriel Magalhaes na Thomas Partey.
Arsenal hawaonekani kuwa na shamra shamra za kutoa ofa kwa Martinelli, ambaye mkataba wake dimbani Emirates unadumu hadi Juni 2024.
Washika mtutu wanatazamia kuimarisha safu yao ya ushambuliaji kwani Alexandre Lacazette na Eddie Naketiah wanatazamiwa kumaliza mikataba yao mwishoni mwa mwezi huu.
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!